SnoopaVision Njia Mpya ya Kuangalia Video za Youtube 1

SnoopaVision Njia Mpya ya Kuangalia Video za Youtube

Ni miaka mingi sasa imepita toka watumiaji wa mtandao wa kushare video wa YouTube kutoa maoni yao mbalimbali kuhusu utumiaji wa mtandao huo maarufu duniani. Hivi karibuni kampuni ya google imetangaza kushulikia moja kati ya maombi ya watumiaji wa mtandao wa YouTube kwa kuongeza namna mpya kuangalia video zake katika mtandao huo.

Njia hiyo mpya iliyopewa jina la SnoopaVision ni ni njia mpya ya kuangalia video kwa mfumo wa 360 yani nyuzi 360 hii inakupa uwezo wa kuona pande zote za video hiyo unayoangalia kwenye mtandao huo wa YouTube. Hata hivyo google wamethibitisha kushirikiana na rapper Snoop Dog ambae ni moja kati ya watu walioshiriki kutengeneza na kutoa idea ya kutengeneza technolojia hiyo mpya.

Kwa maelezo zaidi angalia video hiyo hapo juu na pia unaweza kutembelea Blog ya YouTube kwa habari zaidi.

KUMBUKA HAPPY FOOLS DAY

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Sasa Unaweza Kusoma Meseji za Simu yako Kupitia Windows 10 2
Sasa Unaweza Kusoma Meseji za Simu yako Kupitia Windows 10
Next Post
Game Mpya ya Nintendo Kwaajili ya Smartphone Yako 3

Game Mpya ya Nintendo Kwaajili ya Smartphone Yako