Snapchat Yaleta Group Chat Kipindi Hichi cha Siku Kuu

Kampuni ya Snap.inc yaleta group chat kwenye programu ya snapchat kama zawaidi ya siku kuu
Snapchat Snapchat

Kampuni ya Snap.inc kupitia programu yake ya Snapchat, leo imetangaza kuleta sehemu mpya ya Group chat kama zawaidi kwa watumiaji wake kwenye kipindi hichi cha siku kuu.

Mtumiaji wa programu hiyo ataweza kuchat na marafaiki 10 mpaka 16 uku akiwezeshwa kuona aliye online kwenye group kwa kuangalia mwisho kabisa wa ukurasa wa kuchat kwenye programu hiyo. Kama ilivyo vitu vingine kwenye programu ya snapchat, group chat pamoja na picha zote zilizotumwa kwenye group zitafutika baada ya masaa 24.

Advertisement

Vilevile Snap.inc imeongeza kuwa katika kuhakikisha watu wanasherekea sikukuu hizi na programu hiyo kwa aina ya tofauti, Snapchat imeleta pia Scissors na Paintbrush sehemu nyingine za kutengeneza picha ambazo utaweza kutumia picha hizo kama stickers kwenye programu hiyo.

Kwa habari zaidi za teknolojia unaweza kujiunga nasi kupitia page zetu za Facebook, Instagram, Twitter pamoja na Youtube, pia kama unataka kupata habari za teknolojia kwa haraka pindi zitakapo toka unaweza kudownload App ya Tanzania tech kupitia Play store.

Soma habari mbalimbali za teknolojia kutoka tovuti ya Tanzania Tech
Over 7,000 subscribers
Add a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *