Cantact

Jinsi ya Kurudisha Majina yaliopotea Kwenye Simu yako

Je umepoteza simu na unaitaji kurudisha majina yako yaliyopotea au labda umeyafuta kwa bahati mbaya? usijali, zifuatazo ni njia za kurudisha majina yako yaliyopotea kwa kutumia account yako ya Google.

Kwanza kumbuka kwamba nilazima simu yako iwe imesejiliwa na google ili uweze kupata majina yako yalio potea, kama ulisha jisajili na google ni rahisi sana kupata contact zako zilizo potea. Google hutumia technolojia ya “synced” ilikuifadhi majina yako katika server zao, kwahiyo basi kila mara unapoingiza jina jipya katika smartphone yako google ulihifadhi jina ilo kwenye server yao. Kwanjia hii unaweza kupata majina yalio potea, meseji zailizo potea kwa muda usiopungua siku 30.

Ili huweze kupata majina yako unatakiwa ku “Log in” kwenye account yako ya Gmail kwa njia ya Computer kisha katika upande wa kushoto kwenye neno “Gmail” fuatilia menu yote kwa chini utaona neon limeandikwa “Contacts”.

Hapo utaona majina yote uliyo wahi kutumia kwenye Google email pamoja na yale ya kwenye simu yako ulio tumia kwa account hiyo, katika upande huohuo wa kushoto utaona option nyingine nyingi, bonyeza kwenye sehemu iliyo andikwa “More” baada ya hapo menu mpya zitatoke kisha bonyeza “Restore Contacts”.

Utapewa option za niwakati gani unataka kurudisha majina yako, yaani unataka kurudi nyuma lisaa, siku ama wiki (hii utokana na ni lini ulipoteza majina yako) Kisha baada ya kuchagua option hiyo bonyeza “Restore”.

Hapo utakua umerudisha majina yako kwenye simu yako mpya, ingia kwenye Android yako kisha Connect na Internet kisha anagalia contact zako kama zimerudi kwenye simu.

Kwa wale wasio na akaunti za google yani wasio tumia Android Smartphone, kuna application nyingi kwenye google na kwneye mitandao zinazofanya kazi ya kurudisha contact zilizopotea.

Enedlea kupitia blog hii kila siku kujifunza njia hizo na kujua ni application gani bora za kutumia kwa watu wasio na Gmail akaunti.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
kundoa matangazo
Namna ya Kuondoa Matangazo Kwenye Application za Simu yako
Next Post
Namna ya Kusoma Meseji za Whats App Bila Mtu Kujua 1

Namna ya Kusoma Meseji za Whats App Bila Mtu Kujua