Angalia Video ya Note 7 Ikitumika Kama Bomu Kwenye Game ya GTA 5

Kama ulipitwa hii ndio video ya Note 7 ikitumika kama bomu kwenye Mod la Game ya Grand Theft Auto (GTA 5 )
GTA 5 GTA 5

Siku za usoni kumekua na mvutano kati ya mtu mwenye Youtube channel inayoitwa Modded Games na Samsung Electronics ya marekani, walichokifanya watu hao wenye channel hiyo ni kutengeneza Mod (Modification) ya Game la Grand Theft Auto 5 maarufu kama GTA 5 ambapo kwenye mod hiyo ilionekana Mtu akienda kununua silaa kwenye duka linalo uza silaa na mtu huyo allishia kununua Samsung Note 7 ambayo mtu huyo aliitumia kama bomu alipotoka nje ya duka hilo.

Advertisement

Hata hivyo Samsung walifanikiwa kushawishi kampuni ya Google kupitia Youtube kuondoa video hiyo pamoja na kufungua mashitaka kwa mwenye channel hiyo lakini siku chache baadae video hiyo ikarudi tena kwenye channel hiyo ikiwa na maana kuwa mtu huyo mwenye channel hiyo alishinda katika madai hayo yaliyofunguliwa na Kampuni ya Samsung ya nchini marekani.

Nini maoni yako kwa Samsung kuhusu hii ishu..? unaweza kuandika maoni yako hapo chini au unaweza kujiunga na majadiliano kwenye mitandao yetu ya kijamii ya  Facebook, Twitter na Instagram pamoja na Youtube kama unataka kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya Video. Pia kama unataka kupata habari zote za teknolojia kwa haraka unaweza kudownload sasa App yetu ya Tanzania tech kutoka Play Store na hivi karibuni itapatikana kupitia App Store.

Soma habari mbalimbali za teknolojia kutoka tovuti ya Tanzania Tech
Over 7,000 subscribers
Add a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *