Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok 1

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Mmiliki wa kampuni ya X au Twitter Elon Musk, hivi karibuni ametangaza ujio wa mfumo mpya wa akili bandia ambao utakuwa unaitwa xAI Grok.

Mfumo huu ni utakuwa ni mbadala mshindani wa ChatGPT ambayo inatumia lugha model ya GPT (Generative Pre-trained Transformer) na Google Bard, ambayo inatumia Pathways Language Model 2 (PaLM 2).

Kwa mujibu wa Elon Musk, mfumo wa xAI Grok, unakuja na maboresho mbalimbali kama vile uwezo wa kutoa majibu ambayo mfumo wa ChatGPT au Google Bard haziwezi kutoa. Pia mfumo huo wa akili bandia utakuwa na data mpya ambazo zitakuwa zinatoka kwenye mtandao wa X.

Mfumo wa Grok AI utakuwa unaweza kujibu maswali mbalimbali, na utakuwa ni mfumo wa akili bandia (AI) ambao unajibu maswali kwa kuchangamka, kuchekesha na ukiwa na uwezo wa kufanya utani na mwanadamu. Pia utakuwa na uwezo wa kutumia mfumo huu, mara nyingi kwa wakati mmoja bila kuzidiwa.

Elon amesema tofauti kubwa kati ya Grok na Akili Bandia nyingine kama vile ChatGPT na Google Bard ni kuwa, Grok ina uwezo mkubwa wa kujibu maswali kwa uchangamfu huku ikiweka utani kidogo.

Kwa sasa kwa mujibu wa Elon Musk, mfumo wa AI ya Grok utaanza kupatikana kwanza kwa watumiaji ambao wanalipia kifurushi cha Premium+ katika mtandao wa X au Twitter. Pia unaweza kujiunga kusubiri ili kuwa wa kwanza kujaribu mfumo huu kupitia link hapa.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
Ifahamu Simu Sahihi Kwa Content Creators 2
Ifahamu Simu Sahihi Kwa Content Creators
Next Post
Kutana na Gari Kubwa Kuliko Yote Duniani (Linatembea) 3

Kutana na Gari Kubwa Kuliko Yote Duniani (Linatembea)