Popular Now
Samsung Will Discontinue its Messages app in July 2026 1

Samsung Will Discontinue its Messages app in July 2026

Samsung Yabadilisha Viwango Vya Faragha Ya Simu Duniani Kwa Kuzindua Galaxy S26 Ultra 2

Samsung Yabadilisha Viwango Vya Faragha Ya Simu Duniani Kwa Kuzindua Galaxy S26 Ultra

Sasa Unaweza Kutengeneza Muziki Kupitia Google Gemini 3

Sasa Unaweza Kutengeneza Muziki Kupitia Google Gemini

Hatimaye Nchi ya Misri Yazindua Mtandao Wake wa Kijamii 4

Hatimaye Nchi ya Misri Yazindua Mtandao Wake wa Kijamii

Wakati kampuni ya Facebook ikiendelea na sakata la kuvujisha data za watumiaji wake zaidi ya milioni 50 kupitia kampuni ya Cambridge Analytica, huko nchini Misri mambo ni tofauti kidogo kwani wiki moja iliyopita serikali nchini humo imezindua mtandao wa kijamii maalumu kwaajili ya nchi hiyo.

Mtandao huo mpya unaofanana na Facebook umezinduliwa nchini Misri, kwa jina la EgFace. Hata hivyo mtandao huo wa kijamii unaonekana kutengenezwa mara baada ya Waziri wa mawasiliano nchini Misri kutangaza kuwa Misri itazindua mtandao wake wa kijamii.

Hata hivyo ripoti zinasema, Raia wa Misri walionyesha kukejeli na kutounga mkono uamuzi huo uliotangazwa tarehe 12 mwezi Machi, wengi wao wakiwa na mawazo kuwa, hatua hiyo ni ya makusudi kuwezesha vyombo vya usalama kufuatilia watumiaji wa mtandao huo , kukusanya taarifa na kufuatilia anuani za watumiaji.

Kwa sasa mtandao huo unapatikana kupitia anuani ya egface.com na tayari kuna watumiaji wa chache kutoka nchini humo wamesha anza kutumia mtandao huo, huku ikisemekana kuwa anuani nyingi za mtandao wa Facebook zimefungwa hivi karibuni na tayari watu wengine wamekamatwa kwa makosa ya ”uchochezi” dhidi ya serikali ya Misri,Jeshi na Polisi.

Previous Post
Simu bora za Infinix (2018)

Simu Bora za Infinix Bei Zake na Mahali Pakununua (2019)

Next Post
Apple Yazindua Mfumo wa iOS 11.3 Wenye Maboresho Mapya 5

Apple Yazindua Mfumo wa iOS 11.3 Wenye Maboresho Mapya