Android Kwenye PC

Njia Rahisi na Bora ya Kutumia Android Kwenye PC

Wengi wetu tumesha zoea ya kua ukitaka kutuma android kwenye kompyuta yako ni lazima sana kuwa na programu ijulikanayo kama Bluestack au programu zingine ambazo nyingi huja zikiwa na viambatanisho ambavyo ni lazima kulipia ndipo uweze kutumia, yote hayo kwa sasa ni kwaheri.. Leo Tanzania tech inakuletea njia mpya na rahisi ya kutumia android kwenye kompyuta yako bila kulipia kitu chochote, kwa kufuata njia hii utaweza kudownload game za aina zote kutoka Play Store pia programu mbalimbali nazo utaweza kudownload moja kwa moja kwenye kompyuta yako, basi bila kupoteza muda let’s goooh..

Hatua ya kwanza kabisa na muhimu ni kuhakikisha unatumia kompyuta yenye sifa zifuatazo, hakikisha kompyuta yako inatumia Windows 7 (64-bit) au zaidi pia haikikisha kompyuta yako inatumia processor ya kuanzia Core i3 (au ukiwa na Core i5 na Core i7 ni vizuri zaidi) pia hakikisha ram inafikia japo GB4, kingine cha msingi ni hakikisha kuwa kompyuta yako inayo nafasi japo GB8 na kuendela (GB16 ni vizuri zaidi), cha mwisho kabisa ni Internet hakikisha una bando kwenye Modem yako kuanzia GB 1 na kuendela (hii ni kwaajili ya kudownload programu). Baada ya kuhakiki hayo yote sasa moja kwa moja twende tuka install Android kwenye kompyuta yako.

Hatua ya kwanza bofya HAPA ili kudownload programu ya Remix OS Player, hakikisha una bando la kutosha na kompyuta yako imetimiza vigezo vyote vinavyotakiwa. Baada ya hapo fuata maelekezo kwenye video

Ukisha mailza hatua zote bila shaka utakua umeweza kutumia android kwenye pc yako billa kulipia kitu chochote, ili kuendela kujifunza njia nyingine mbalimbali za kutumia android kwenye kompyuta yako endelea kutembelea blog ya tanzania tech kila siku au unaweza kupata habari zote za teknolojia moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kwa ku-download App ya Tanzania tech  moja kwa moja kwenye simu yako ya Android, pia unaweza kujiunga nasi kwa barua pepe pamoja na mitandao yetu ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram pamoja na Yotube kwa kujifunza mambo mbalimbali ya teknolojia kwa njia ya video.

Comments

No comments yet. Be the first!

Previous Post
google-pixel
Google Pixel Ndio Simu Yenye Nguvu Mwaka Huu
Next Post
samsung-galaxy-note-7

Samsung Galaxy Note 7 Kurudi Sokoni September 28