Instagram na Facebook Kuanza Kuuza Alama ya Verification

Hivi karibuni utaweza kununua alama ya verification Instagram, Facebook
Instagram na Facebook Kuanza Kuuza Alama ya Verification Instagram na Facebook Kuanza Kuuza Alama ya Verification

Wakati Twitter ikitegemea kuruhusu watumiaji wake kutoka nchi zote duniani kununua alama ya Verification, Habari mpya jumapili ya leo ni kuwa kampuni ya Meta nayo ambayo ina miliki mitandao ya Facebook, WhatsApp na Instagram imetangaza kuanza kuuza alama ya Verification.

Maarufu kama “Blue Tick” alama ya verification imekua kama muongozo wa kujua kurasa au page za watu maarufu au kampuni mbalimbali.

Lakini kupitia ukurasa wake wa Facebook Mark Zuckerberg, ametangaza kuwa hivi karibuni huduma ya Meta Verified inatarajiwa kuanza na watumiaji wataweza kununua alama ya Verification moja kwa moja.

Advertisement

Kwa mujibu wa Mark Zuckerberg Instagram na Facebook inategemea kuanza kuuza verification kuanzia dollar $11.99 ambayo ni sawa na TZS 30,000 kwa watumiaji kupitia browser, dollar $14.99 sawa na TZS 35,000 kwa watumiaji wa iOS.

Pia mtumiaji anatakiwa kuwa na kitambulisho ili kuweza kununua alama ya verification, alama ambayo itasaidia mnunuaji kupata huduma kwa wateja haraka, pamoja na kuongeza ulinzi zaidi kwenye kurasa au page usika.

Kwa sasa bado hakuna taarifa za lini huduma hii itakuja kwa watumiaji wa simu za Android, huku Mark akitangaza kuwa huduma hii inategemea kuanza wiki hii kwa nchi za Australia na New Zealand huku nchi nyingine zikifuatia baadae.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use