in

Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui

Shortcuts hizi zina weza kufanya kazi kwenye toleo lolote la Windows 7, 10 au 11

Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui

Pamoja na kuwa kwa sasa kila kitu kinaweza kufanyika kwenye simu lakini ni wazi kuwa bado kompyuta zinazo nafasi yake kwa kiasi chake. Kuliona hili leo nimekuletea makala hii fupi ya shortcuts za windows ambazo unaweza kutumia kwenye kompyuta yako.

Inawezekana kwa namna moja ama nyingine ulikuwa hujui kuhusu shortcuts hizi hivyo ningependa usome makala yote hadi mwisho kwani naamini utaweza kujifunza mambo mengi sana kuhusu shortcuts za Windows. Basi bila kupoteza muda twende moja moja.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Window Key + V

Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui

Kwa kutumia shortcuts hii utaweza kufungua clipboard ambapo utaweza kuona maandishi au kitu chochote ulicho copy. Uzuri wa njia hii unaweza kuona vitu zaidi ya kimoja ambacho uli copy awali au mwanzo kabla ya kufanya shortcuts hii.

Ctrl + Shift + V

Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui

Shortcut hii inaweza kusaidia kucopy kitu na kupaste kikiwa plain text, yaani kama umecopy kitu au maandishi yenye rangi na unataka kupaste hicho kitu bila rangi hiyo basi unaweza kutumia shortcuts hiyo kwa kubofya Ctrl + Shift + V.

Ctrl + S

Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui

Shortcut hii ni kwaajili ya kusave kitu chochote ambacho ulikuwa unafanya, kama ulikuwa una andika document yoyote na unataka kusave kwa haraka basi moja kwa moja unaweza kubofya Ctrl + S kwenye keyboard yako na moja kwa moja utaweza kusave document yako.

Ctrl + Z

Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui

Kupitia shortcut hii unaweza kufuta kitu chochote ambacho umefanya awali yani kwa lugha ya kompyuta ni Undo. Sehemu hii inaweza kutumiwa wakati una andika document yoyote pia ndani ya programu mbalimbali pamoja na tovuti. Pia unaweza kutumia Ctrl + Y kuredo au kuredisha chochote ambacho ulifanya awali.

Alt + F4

Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui

Kupitia shortcut hii utaweza kufunga programu au kitu chochote kilichopo juu ya kompyuta yako. Unaweza kufanya hii muda wowote lakini kuwa makini kwa kama hujasave kitu unachofanya kwani shortcuts hii inaweza kufunga programu au window unayotumia moja kwa moja.

Ctrl + F5

Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui

Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao kwa muda mrefu shortcut hii inaweza kusaidia sana, unaweza ku-refresh page ambayo ina matatizo yoyote. Utaweza kufanya page ambayo haifanyikazi vizuri au haifunguki kwa haraka, hii inatumika zaidi kwenye mtandao au web browser.

Alt + Tab

Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui

Kama unataka kubadilisha Tab kwa haraka, hii ni kama unataka kubadilisha kazi moja na nyingine kwa haraka yani kwa mfano kama umefungua document mbili au zaidi ambazo unataka kusoma kusoma zote kwa pamoja unaweza kutumia njia hii kwa urahisi na haraka.

Windows Key + Tab

Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui

Hii ni aina nyingine ya kufungua Tab na ambayo inafanya kazi zaidi kwenye Windows 10 unaweza kufungua timeline ya kila kitu ambacho unafanya au umekifungua kwenye kompyuta yako kwa muda huo, unaweza kuona kila kitu kwa mstari.

Windows Key + Mshale Wowote

Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui

Kama unataka kusogeza kioo cha kompyuta yako kushoto au kulia unaweza kutumia shortcuts hii ambayo inaweza kukusaidia pia kugawa kompyuta yako kwa urahisi na haraka. Njia hii ni nzuri kama unataka kufanya kazi nyingi au zaidi kwa wakati mmoja.

Windows Key + D

Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui

Shortcut hii inakusaidia kama unataka kuficha kila kitu kilichopo kwenye kioo cha kompyuta yako, hii ni nzuri kama unataka kuficha kwa hara kila kitu kichopo juu ya kioo chako ili mtu yoyote asiweze kuona. Unaweza kubofya mara mbili kurudisha vitu vilivyoficha kwa mara ya kwanza.

Windows Key + Namba

Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui

Kama unataka kufungua programu yoyote iliyopo kwenye tab kwa chini kwa haraka unaweza kufanya hivyo kwa kubofya kitufe cha windows kisha chagua namba kulingana na programu unayotaka kufungua. Kwa mfano kama unataka kufungua programu ya kwanza basi bofya Window key + alafu bofya namba 1. Pia unaweza kurudia kuweza kufunga programu husika.

Ctrl + Shift + T

Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui

Kupitia shortcut hii utaweza kufungua tab zote ambazo umezifunga kwenye kompyuta yako yaani kama kwa bahati mbaya umefunga browser yako kwa bahati mbaya unaweza kutumia shortcut hii kuweza kufungua tena ulichokifunga kwa bahati mbaya.

Shift + Windows key + S

Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui

Kama unataka kuchukua screenshot kwenye kompyuta yako kwa haraka na kama unataka kuchugua sehemu hiyo ya kuchukua screenshot basi unaweza kubofya kitufe cha Windows kisha bofya shift alafu bofya S, kisha chagua sehemu ambayo unataka kuscreeshot kwa kutumia mause ya kompyuta yako.

Windows Key + E

Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui

Ni wazi unajua kuwa Windows 10 haiji moja kwa moja na sehemu ya my computer, lakini unaweza kuwasha sehemu hii kwenye settings kama unataka, lakini kama unaona shida kutafuta sehemu hiyo kwenye settings basi unaweza kubofya Windows key + E kisha utaona My computer imefunguka au recently file inategemeana na settings za kompyuta yako.

Na hizo ndio shortcut za Windows ambazo nimekuandalia kwa siku ya leo, unaweza kuendelea kujifunza zaidi kwa kusoma hapa jinsi ya kuinstall Windows 10 kwa kutumia simu yako ya Android. Kama unataka kujifunza zaidi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

Shortcuts (14) za Windows Ambazo Ulikuwa Huzijui
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kufuta kwa Haraka Majina Yaliyo Jirudia

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment