TECNO Yakabidhi Zawadi kwa Mshindi wa Promosheni ya Spark 8C

TECNO imehitimisha rasmi promosheni ya simu ya SPARK 8C baada ya kukabidhi zawadi ya Milioni 5
TECNO Yakabidhi Zawadi kwa Mshindi wa Promosheni ya Spark 8C TECNO Yakabidhi Zawadi kwa Mshindi wa Promosheni ya Spark 8C

Kampuni ya simu ya TECNO imehitimisha rasmi promosheni ya simu ya SPARK 8C baada ya kukabidhi zawadi ya milioni 5 pesa taslimu za kitanzania kwa mshindi anayefahamika kwa jina la Mohammed Khatibu.

TECNO Yakabidhi Zawadi kwa Mshindi wa Promosheni ya Spark 8C

Meneja mauzo TECNO akiwa anaelezea kuhusu promosheni ya SPARK 8C

Advertisement

Meneja Mauzo wa TECNO, Bi. Mwamvua Hussein Kapesula alizungumza na kusema, “Niko mbele yenu leo kukabidhi zawadi ya shilingi milioni 5 kwa mshindi wa promosheni ya SPARK 8C ambaye ni ndugu Mohammed Khatibu.

TECNO Yakabidhi Zawadi kwa Mshindi wa Promosheni ya Spark 8C

Meneja Mauzo wa TECNO akiwa anakabidhi zawadi kwa mshindi

Promosheni hiyo ilizinduliwa rasmi mnamo mwezi April na kudumu kwa muda wa mwezi mmoja na mshindi alitangazwa live kupitia @tecnomobiletanzania mnamo tarehe 24/05/2022.

Ndugu Mohammed Khatibu ambaye ndiye mshindi wa promosheni hiyo alionyesha furaha yake kwa kusema “Kwa kweli nilijiskia furaha kubwa baada ya TECNO kunipigia simu na kunieleza nimeshinda millioni 5 baada ya kununua simu ya SPARK 8C na hatimaye leo kukabidhiwa zawadi hiyo. Nilikuwa na ndoto ya kufungua maabara yangu na napenda kuwashukuru TECNO kwa kuwa sehemu ya kufanikisha ndoto yangu hiyo”.

TECNO Yakabidhi Zawadi kwa Mshindi wa Promosheni ya Spark 8C

Ndugu Mohammed Khatibu akiwa amekabidhiwa zawadi

Kadhalika, afisa mahusiano wa TECNO, Bi. Prisca Ernest alitoa shukrani zake kwa kusema, “Shukrani nyingi ziwafikie wateja wetu wote wa TECNO walioweza kufika katika maduka yetu yote nchini Tanzania na kununua simu hii ya SPARK 8C na hata simu zetu nyingine pia”.

TECNO Yakabidhi Zawadi kwa Mshindi wa Promosheni ya Spark 8C

Wafanyakazi wa TECNO wakiwa na hundi ya mshindi

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use