in

Apps za Kudownload Mafile Makubwa kwa Haraka (Android)

Download mafile ya aina zote kwa haraka kwenye simu yako kwa kutumia app hizi

Apps za Kudownload Mafile Makubwa kwa Haraka (Android)

Ni wazi kuwa teknolojia ya simu hasa smartphone inaendelea kukuwa kwa kasi kubwa sana, watu wamekuwa wakifanya kila kitu kwa kutumia smartphone lakini bado kuna baadhi ya mambo ni lazima kutumia kompyuta ili kufanya kwa haraka.

Kwa mfano, ni wazi kuwa imekua ni mthiani sana kudownload mafile mbalimbali makubwa kupitia kwenye simu yako ya Android kwa haraka kama ilivyo kudownload kupitia kwenye kompyuta.

Kuliona hili leo nimekuletea apps ambazo zitakusaidia sana kudownload mafile makubwa kwenye simu yako ya Android kwa haraka na kwa urahisi kama ambayo inakuwa kwenye kompyuta. Kupitia apps hizi utaweza kupakua mafile yote kwa urahisi bila kutumia muda mrefu.

Basi bila kuendelea kupoteza muda wako zaidi, moja kwa moja twende nikuonyeshe apps hizi ambazo na uhakika zitakusaidia sana.

Advanced Download Manager & Torrent downloader

Apps za Kudownload Mafile Makubwa kwa Haraka (Android)

Kama wewe umekuwa ni mtu ambae unapenda kudownload movie na mafile mengine mekubwa kwenye simu yako basi pengine Advanced Download Manager & Torrent downloader ni app bora sana kwako kutumia.

Apps Nzuri za Kufuatilia kwa Karibu Kombe la Dunia

App hii inaweza kupakua mafile makubwa kwa vipengele ikiwa pamoja na uwezo wa kusubirisha file na kudownload pale utakapo pata MB. Pia unaweza kudownload kidogo kidogo kulingana na MB zako, mbali na hayo pia utaweza kudownload movie kupitia Torrent kwa urahsi na haraka.

Download App Hapa

1DM+ : Video, Torrent Downloader

Apps za Kudownload Mafile Makubwa kwa Haraka (Android)

App nyingine ambayo itakusaidia kudownload kwa haraka kupitia kwenye simu yako ya android ni 1DM+, app hii pia itakuwezesha kudownload mafile makubwa kwa kuweza kuyasubirisha pale utakapo ishiwa na bando (ku-pause), ikiwa pamoja na uwezo wa kudownload movie na video kwa haraka kutoka kwenye tovuti zote za Torrent.

Kitu kingine bora kuhusu app hii pia utaweza kudownload kwenye kurasa zenye matangazo bila kuweza kuangalia matangazo kwani app hii inaweza kuzuia matangazo moja kwa moja.

Download App Hapa

Navi Download Manager

Apps za Kudownload Mafile Makubwa kwa Haraka (Android)

Navi download manager ni app ya mwisho kwenye list hii fupi, app hii ni nzuri na inaweza kusaidia sana kudownload mafile makubwa kwa haraka na kwa kuweza kupause. Mbali ya kuwa app hii inaweza kufanya yote hayo pia app hii ni Open Source hii ina maana kuwa unaweza kudownload code za app hii na kutengeneza app yako kwa kutumia code hizi na kuweka Play Store.

Apps za Kusaidia Kujibu Meseji WhatsApp (Bila Kushika Simu)

Kama unataka kutengeneza app yako ambayo unataka iwasaidie watu kudownload kwa haraka unaweza kupakua Source code za app ya Navi Download Manager hapa, pia kama unataka kujaribu app hii basi unaweza kudownload kupitia link hapo chini.

Download App Hapa

Na hizo ndio app ambazo zitakusadia kudownload mafile makubwa kwa haraka kupitia simu yako ya Android. Kama unataka kujua zaidi unaweza kusoma hapa kujua app bora ambayo inaweza kukusaidia kudownload video zote za kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter na mitandao mingine.

Kama unataka kuendelea kujifunza kila siku hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania tech kila siku ili ujifunze zaidi kuhusu teknolojia.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.