in ,

Jiandae na Simu Mpya ya Infinix NOTE 11 Pro Hapa Tanzania

Jiandae na toleo jipya la simu za Note kutoka kampuni ya Infinix

Jiandae na Simu Mpya ya Infinix NOTE 11 Pro Hapa Tanzania

Kampuni ya simu ya Infinix ilizindua rasmi Infinix NOTE 11 na Infinix NOTE 11 Pro mwanzoni mwa mwezi October huko Ugaibuni.

Infinix NOTE 11 Pro ni simu ya kwanza kwa kampuni ya simu Infinix kuja na Gaming processor ya MediaTek Helio G96 na Ram ya GB8 na GB3 ya memory ya ziada.

Jiandae na Simu Mpya ya Infinix NOTE 11 Pro Hapa Tanzania

Kulingana na uchambuzi uliofanywa na blog kuwa ya tech duniani ‘Gadgets’ ni dhahiri Infinix NOTE 11 pro ni simu ambayo inaweza kufanya kile ambacho computer ingefanya kwa speed ile ile.

Kupitia mifano mbalimbali ya simu za awali za Infinix inasemekana Infinix NOTE 11 Pro si kwamba tu ni simu ya kwanza kuja kuwa na speed kubwa zaidi wa ufanyaji kazi za kiofisi na kucheza games za ujazo mkubwa kwa muda mrefu pasipo simu kupata moto lakini pia itakuwa simu ya kwanza ya series ya NOTE kuwa na kioo chenye refresh rate ya haraka zaidi na kumfanya mtumiaji afurahie wakati wa kuperuzi application mbalimbali.

Fahamu eSIM Mfumo Mpya wa Laini za Simu za Kidigitali

Jiandae na Simu Mpya ya Infinix NOTE 11 Pro Hapa Tanzania

Ukichungulia page ya instagram ya @infinixmobiletz unaona ni namna gani simu hii imeweza kuzua taharuki idadi kubwa ikitamani kujua bei ya simu hiyo fununua zinadai kuwa Infinix NOTE 11 pro itapatikana kwa bei rafiki kabisa ya sh. 600,000 za Kitanzania lakini kwa mteja wa pre-order atapewa punguzo la sh.50,000

Kaa tayari kupokea mzigo huu nchini Tanzania mwishoni mwa mwezi October.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.