in ,

Hizi Hapa Programu (4) za Kuflash Simu za Android (2021)

Tumia programu hizi kuflash simu za Samsung, Tecno, Infinix, iTel pamoja na Nokia

programu za kuflash simu

Imekuwa ni kitu cha kawaida sana siku hizi kwa watumiaji wa simu kuflash simu zao wenyewe, iwe ni kwa sababu ya kuondoa matatizo mbalimbali ya simu husika au kwa kufanya marekebisho fulani.

Kuflash simu imekuwa sio tatizo la kupeleka simu yako kwa mtaalamu, Lakini japokuwa kuflash simu ni kitu cha kawaida na kirahisi lakini bado kuna tatizo juu ya upatikanaji wa programu za kuflash simu mbalimbali za Android.

Sasa kuliona hili leo hapa Tanzania Tech tumekukusanyia programu maalum za kuflash simu ikiwa pamoja na link maalumu za kudownload programu hizo. Kumbuka, programu hizi zina tofautiana kwenye kila simu hivyo ni muhimu kusoma kwa umakini kabla uja download programu husika.

Programu za Kuflash Simu

Programu hizi za kuflash simu zina tofauti kwa matumizi hivyo ni muhimu sana kuhakikisha unafuata maelezo ya jinsi ya kutumia programu hizo kwa usahihi ili usije kuharibu simu yako.

Pia ni muhimu kukumbuka kuflash simu yako kunaweza kuharibu baadhi ya mikataba kama vile warranty pamoja na mikataba mingine ya sehemu uliyo nunulia simu yako, hivyo kumbuka kuwa unafanya hivi kwa kutambua madhara ya kuflash simu yako.

Jinsi ya Kuforward Simu Moja kwenda Nyingine (Kudivert)

SamFirm – Simu za Samsung

Hizi Hapa Programu (4) za Kuflash Simu za Android (2021)
Muonekano wa programu ya SamFirm

SamFirm hii ni programu ya mfumo wa Windows ambayo inatumika kuweza kudownload kwa haraka pamoja na kutafuta firmware za simu za Samsung. Programu hii ni bora sana kwa sababu inasaidia kupata Firmware halisi ya simu yako na pia utaweza kudownload firmware kwa haraka bila kukata kata.

Sasa kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanataka kuflash simu za Samsung basi unaweza kutumia programu hii kuweza kudownload Firmware ya simu yako.

Download SamFirm Hapa

Odin – Simu zenya Snapdragon

Kama wewe ni mtumiaji wa simu ya Samsung, programu ya Odin ni muhimu wewe kuifahamu. Programu hii inauwezo wa kuflash tablet na simu mbalimbali za Samsung hata zile ambazo ni mpya kabisa kama vile Samsung Galaxy S9 na nyingine kama hizo.

Programu hii ya kuflash simu haiuzwi na ni bure kabisa kutumia unachotakiwa ni kuwa na Firmware ya simu yako ya Samsung ambayo unaweza kuipata hapa, programu ya kuflash simu ya Odin unaweza kuidownload kupitia link hapo chini.

Download Odin Hapa

SP Flash Tool – Tecno, Infinix, iTel na Simu za China

Hizi Hapa Programu (4) za Kuflash Simu za Android (2021)
Muonekano wa SP Flash Tool

Kama wewe ni mtumiaji wa simu za TECNO, Infinix na simu nyingine kama hizo ambazo zinatumia chipset ya MediaTek basi ni vyema kufahamu programu hii ya kuflash simu.

Tovuti za Kujifunza Kutengeneza Apps na Website Bure 100%

Programu hii inaweza kuflash simu nyingi za kutoka nchini china na pia kama ilivyo programu ya kwanza kwenye list hii programu hii pia ni bure kabisa kudownload na pia ni bure kabisa kutumia, kitu cha msingi unachotakiwa kufanya ni kuwa na Firmware ya simu yako ambayo unaweza kuipata hapa. Kwa programu ya SP Flash tool unaweza kupakua kupitia link hapo chini.

Download SP Flash Tool Hapa

Phoenix Suit – Nokia za Zamani

Hizi Hapa Programu (4) za Kuflash Simu za Android (2021)
Muonekano wa Phoenix Suit

Kama wewe ni mmoja wa watu wanaotumia simu za Nokia za zamani basi ni vyema kufahamu programu hii ya Phoenix Suit, programu hii inauwezo wa kuflash simu mbalimbali lakini zaidi inauwezo wa kuflash simu za Nokia. Unaweza kuipata programu hii bure kabisa kupitia link hapo chini.

Download Phoenix Suit Hapa

Hitimisho

Na hizo ndio programu za kuflash simu ambazo unaweza kutumia kuflash simu yako, programu hizi ni baadhi tu ambazo zimethibitika kuweza kufanya kazi vizuri, kama kuna programu nyingine ambayo itajitokeza siku za karibuni basi moja kwa moja tutaiongeza hapa kwenye makala hii.

Kuhakikisha hupitwi na habari yoyote hakikisha una jiunga na channel yetu ya Tanzania Tech kupitia hapa.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

28 Comments

  1. Nilikuwa naomba kujuwa jisi ya kuondoa I clud clock kwenye I phone ndug mume kuwa msa ada kwang San n nipo papoja na nyie mupo vizur kwa technology naitaj msa Ada wenu hap nyins ya kutoa I clod clok Kweny I phon

  2. Nina simu ya huwawei y520-u22 nijaribu kuiflashi inagoma file nimedownload lakini imeshindikana maanake file za simu zinaandika unfortunately stopped nisaidie shida yake niipi? au nitumie njia gani ili ipone

  3. Lakin pia kompyuta yangu inasumbua sana maana inadai ku activate lakin Sijajua ku download kmspico nakila nikijaribu kudownload kwenye Sm lakin nikiweka kweny kompyuta inagoma kufanya kazi na kompyuta yangu inasumbua sn hadi Kwasas kuna badh y program azifany Kaz naitaj San msa Ada web