Futa Haraka Apps Hizi Kwenye Simu Yako ni Hatari

Apps hizi ni hatari na zinaweza kuhatarisha usalama wa simu yako na data zako
Futa Haraka Apps Hizi Kwenye Simu Yako ni Hatari Futa Haraka Apps Hizi Kwenye Simu Yako ni Hatari
©sophos.com

Kama wewe ni msomaji wa tovuti ya Tanzania Tech ni wazi kuwa unajua kuwa mara nyingi tumekuwa tunaongelea zaidi kuhusu apps nzuri za kuinstall kwenye simu yako. Lakini kwa siku ya leo tunaenda kuongelea kinyume chake.

Kupitia makala hii tutaenda kuangalia apps ambazo ni hatari kwa simu yako na ambazo kwa ushauri wangu ningependa uzifute haraka sana kwenye simu yako. Najua unataka kujua app hizi hivyo moja kwa moja twende kwenye list hii.

Apps za Free VPN

Futa Haraka Apps Hizi Kwenye Simu Yako ni Hatari

Advertisement

Hivi karibuni kuwa kuwa na matumizi makubwa sana ya VPN hasa hapa Tanzania, lakini mbali ya kuwa VPN ni kiungo muhimu wakati wa kutumia Internet ni wazi kuwa zipo apps za Free VPN ambazo sio salama hata kidogo.

Kwa mujibu wa tovuti ya thenextweb, apps nyingi za Free VPN zina mtindo wa kuuza data za watumiaji ili kutengeneza pesa. Mbali na hayo apps hizi sio salama kutokana na kuwa miundo mbinu inayotumika sio salama na hivyo kuongeza uwezekano wa data zako kudukuliwa kwa urahisi.

Apps za Kuongeza RAM

Futa Haraka Apps Hizi Kwenye Simu Yako ni Hatari

Miaka ya nyuma wakati mfumo wa Android unaanza kutumika ni wazi kuwa apps za kuongeza uwezo wa RAM zilikuwa maarufu sana. Baadhi ya apps hizo zilikuwa zinaonekana kufanya kazi lakini sio zote.

Miaka mingi mbele, mfumo wa Android sasa umeboreshwa na hakuna simu yoyote ambayo inazinduliwa sasa yenye uhitaji wa app yoyote ya kuongeza uwezo wa RAM. Hivyo uhitaji kabisa kupakua apps zenye kudai kuongeza uwezo wa simu kufanya kazi kwa haraka kwani kinachotokea hapo ni kitu tofauti kabisa.

Kwa mujibu wa beebom, baadhi ya apps hizi huchukua data zako za muhimu kutoka kwenye file mbalimbali ambazo inadai inazifuta hivyo kama unatumia simu ya kisasa huna haja kabisa ya app hizi zinazodai kuongeza uwezo wa RAM kwani simu nyingi za sasa zinakuja na sehemu ya kufuta apps zinazo chukua nafasi kubwa kwenye simu yako.

Apps Zenye Kutaka Ruhusa Nyingi

Futa Haraka Apps Hizi Kwenye Simu Yako ni Hatari

Ni wazi kuwa ili app yoyote iweze kufanya kazi kwenye simu yako inahitaji ruhusa fulani au permission. Lakini zipo baadhi ya apps ambazo zinahitaji ruhusa nyingi kupitia uwezo wa app. Kwa mfano unakuta unataka kufungua game fulani kwenye simu yako na unaona inahitaji permission nyingi kama vile uwezo wa kuona namba zako za simu, mahali ulipo (location) na nyingine nyingi.

Ukiangalia Game haina haja ya kupata ruhusa ya kuona namba zako za simu, na pia kama game hiyo haina michezo ya live haina haja ya kuomba ruhusa ya location au ruhusa nyingine ambazo unaona hazihitajiki.

Mbali na games pia zipo apps nyingi ambazo pia zinahitaji ruhusa ambazo sio za lazima kwenye app husika. Kama unatumia simu yenye mfumo mpya wa Android 11, na ni muhimu kwa wewe kuruhusu app fulani kutumia permission fulani basi tumia sehemu ya Allow only once.

Hitimisho

Hizi ni baadhi tu ya apps ambazo ni muhimu kuondoa kwenye simu yako. Ingawa bado zipo apps nyingi sana ambazo sio salama ni vizuri kuanza na hizi ambazo zinajulikana sana kwa kutokuwa salama.

Kama unataka kujua zaidi kuhusu usalama, unaweza kusoma hapa kujua mambo ambayo hutakiwi kufanya unapo tumia Internet. Kwa habari zaidi hakikisha una tembelea channel yetu ya Tanzania Tech hapa natumaini utaweza kujifunza mambo mengi kuhusu teknolojia.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use