in ,

Jinsi ya Kuzima Bluetooth Kwenye Android TV Yoyote

Utaweza kuzima bluetooth kwenye Smart TV yoyote inayotumia mfumo wa Android

Jinsi ya Kuzima Bluetooth Kwenye Android TV Yoyote

Kama wewe ni mmoja wa wamiliki wa TV za Android basi ni wazi kuwa umeshakutana na tatizo la bluetooth kuwa ON kila wakati na hii kufanya watu (majirani) kujaribu kuunganisha bluetooth kwenye TV yako kila mara bila ruhusa na kusumbua TV yako na jumbe za ku-pair bluetooth.

Kama unavyojua TV nyingi za Android hazina sehemu za kuzima bluetooth hii inatokana na teknolojia hiyo kutumiwa sana kwenye TV hizi hivyo kutokuwa na ulazima wa kuzima bluetooth. Japokuwa hata kama bluetooth ikiwa ON bado TV yako ni salama lakini hii ni hadi pale mtu atakapo fanikiwa ku-pair kwenye TV yako.

Jinsi ya Kuzima Bluetooth Kwenye Android TV Yoyote

Sasa kuondoa matatizo ya husumbu na usalama leo nimekuletea njia mpya ya kuweza kuzima bluetooth kwenye TV yako ya Android kwa urahisi na haraka.

Kwa kuanza moja kwa moja unachotakiwa kufanya ni kudownload app hapo chini, app hii ina KB 400 hivyo ni rahisi kwako kudownload, unaweza kudownload app hii moja kwa moja kwa moja kwa kupitia TV yako au unaweza kudownload kwa kutumia simu yako kisha hamishia kwenye kompyuta yako.

Jinsi ya Kupata Email au Barua pepe ya Mtu Yoyote Kwa Urahisi

Download App Hapa

Baada ya kudownload app hii na kuinstall kwenye TV yako ya Android moja kwa moja fungua app hii na utaona muonekano kama huo hapo chini.

Jinsi ya Kuzima Bluetooth Kwenye Android TV Yoyote

Baada ya hapo chagua settings kulingana na mahitaji yako ya muda huo, unaweza kuchagua kulingana na maelekezo hapo chini.

  • Fully discoverable and pairable – ukichagua sehemu hii bluetooth itakuwa ON kila wakati na TV yako itakuwa inaonekana pale mtu atakapo search bluetooth kwenye simu au kifaa chochote chenye bluetooth.
  • Limit to devices that are already discovered – Kwa kuchagua sehemu hii utaweza kuruhusu vifaa ambavyo tayari unanavyo viona kwa sasa kwenye TV yako na sio vifaa vipya.
  • Limit to devices that are already paired – Kwa kuchagua sehemu hii utaweza kuruhusu vifaa ambavyo tayari ulisha viunganisha kwenye TV yako na sio vifaa vipya.
  • Completely disable Bluetooth – Kwa kuchagua sehemu hii utaweza kuzima kabisa bluetooth na vifaa vyote vipya na vya zamani havitaweza kuunganisha kwenye TV yako.
Jinsi ya Kutumia Smartphone Yako Kama Microphone

Kwa hiyo basi kama unataka kuzima kabisa bluetooth kwenye TV yako ya Android basi unaweza kuzima kwa kuchagua sehemu ya mwisho kabisa kwenye app hii.

Bila shaka sasa utakuwa umeweza kuzima bluetooth kwenye TV yako ya Android na hautoweza tena kupata usumbufu wowote. Kumbuka njia hii inafanya kazi kwenye smartTV yoyote yenye mfumo wa Android.

Kujua zaidi umuhimu wa hili, unaweza kusoma hapa mathara ya kuacha bluetooth ON kwenye kifaa chako kama vile smart TV, smartphone na vifaa vingine. Kwa maujanja zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.