in

Jinsi ya Kuona Namba za Simu za Mtu Unaechati Nae Facebook

Pia unaweza kupata namba za simu za watu ambazo ulizipoteza

Jinsi ya Kuona Namba za Simu za Mtu Unaechati Nae Facebook

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatumia sana mtandao wa Facebook basi najua hadi sasa unajua kuwa ni muhimu sana kuhakikisha unakuwa salama hasa ukiwa kwenye mtandao huo.

Hii ni kwa sababu hakuna usalama wa mtandao wenye uhakika wa asilimia 100 hivyo ni muhimu kuchukua jitihada za binafsi kuweza kujiweka salama mwenyewe.

Sasa kuliona hili leo nataka nikuonyeshe njia fupi sana ambayo lengo lake ni kukujulisha kuwa, sio kila kitu ambacho app yoyote inakuuliza wewe unaharakisha kubofya OK bila hata kujiuliza kwanini app hiyo inataka ruhusa kama hiyo.

Kumbuka njia hii sio udukuaji bali sehemu hii ipo wazi kwa asilimia 100 na mtu yoyote anaweza kuingia sehemu hiyo ili kuona namba za simu za mtu.

Sasa hebu tuache maneno mengi kwani nilitangulia kukwambia kuwa makala hii itakuwa fupi kwani najua kwa sasa lazima unayo mambo mengi ya kufanya. Kumbuka njia hii inafanyakazi endapo unayechati naye ameruhusu namba yake ya simu kuonekana hivyo usishange pale utakapo ona namba za simu za watu wachache tu.

Sasa basi kwa kuanza unatakiwa kuwa umeingia kwenye akaunti yako ya Facebook kwa kutumia kivinjari (browser) yako, kisha baada ya hapo chini na moja kwa moja utapelekwa kwenye ukurasa unao fanana na huo hapo chini.

Tembelea Facebook Hapa

Jinsi ya Kuona Namba za Simu za Mtu Unaechati Nae Facebook

Ili kuweza kuona namba ya mtu bofya namba husika na moja kwa moja utaletewa namba kamili, pia kumbuka Facebook ina mtindo wa kuchukua namba zako zilizopo kwenye phonebook yako hivyo usishangae pale utakapo kutana na listi nzima ya namba za simu zilizopo kwenye phonebook yako.

Natumaini hadi hapo umeweza kuona ni jinsi gani unahitaji kuwa muangalifu wakati unatumia mitandao mbalimbali, kitu cha msingi kuwa makini na ruhusa unazotoa kwenye app mbalimbali kwani kuna app nyingine zinahitaji ruhusa ambazo hata sio za ulazima wakati unatumia app hiyo.

Unacho takiwa kufanya ni kujaribu kukataa baadhi ya ruhusa pale unapoona app inaomba ruhusa ambayo haiendani na aina ya app yenyewe, kama app hiyo ikikataa kufanya kazi basi huenda ruhusa hiyo ni ya ulazima basi hapo huna budu zaidi ya kuruhusu ruhusa hiyo kama unataka kutumia app hiyo.

Lakini wakati mwingine unakuta app nyingi zinaendelea kufanya kazi kama kawaida hata baada ya wewe kukataa kutoa ruhusa hiyo, kwa mfano kwa upande wa facebook messenger jitahidi usiruhusu ruhusa hii (Picha hapo chini) kama unataka namba yako isiweze kuonekana kwenye list ya namba ambazo zinapatikana kwa kutumia njia hii.

Jinsi ya Kuona Namba za Simu za Mtu Unaechati Nae Facebook

Kama unataka maelezo zaidi unaweza kusoma hapa, lakini lama unataka kujua njia za ziada za kuhakikisha akaunti zako za mitandao ya kijamii zinakuwa salama basi hakikisha una soma makala hii hapa ambayo inafundisha kwa video jinsi ya kulinda akaunti zako za mitandao ya kijamii pamoja na kujiweka salama hasa kwa kutumia namba zako za simu.

Soma Hapa Kufahamu Kuhusu CTR, CPC na RPM ya Adsense

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

4 Comments

  1. Kupitia makala hii nimechoka nimechoka na nilichokiona, namba za watu tangu 2015 nimezikuta huko na sikujua nitazipata wapi maana Google contact walipoteza namba zangu zote kwa email asante kaka ila changamoto kuzipakua sasa