in

Jinsi ya Kuongeza Speed ya Internet Kwenye Kompyuta

Kufanya kompyuta yako kuwa na speed mara mbili zaidi ya Internet

kuongeza speed ya internet kwenye kompyuta yako

Kwa namna moja ama nyingine wengi watu hapa ni lazima tumewahi au tunatumia internet kwenye kompyuta, lakini najua pia ni watu wengi sana wanakuwa na tatizo la Internet kuwa na Speed ndogo kwenye kompyuta zao, iwe una download Movie au unafungua tovuti kama Facebook lazima kompyuta yako inakuwa na speed ndogo ya Internet.

Sasa kuliona hili leo hapa Tanzania Tech tunaenda kushirikiana nanyi maujanja ambayo unaweza kutumia ili kuweza kuongeza speed ya Internet kwenye kompyuta yako.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kumbuka njia hizi ni kwaajili ya kompyuta zinazotumia mfumo wa uendeshaji wa Windows 11. Pia kama kompyuta yako haina tatizo la Speed ya Internet lakini iko slow sana, unaweza kusoma hapa mambo yanayosababisha kompyuta yako kuwa slow. Baada ya kusema hayo twende kwenye maujanja ya siku ya leo.

Badilisha au Tumia DNS Servers

DNS kirefu chake ni Domain Name System, sehemu hii ina kazi ya kuweza kubadilisha jina la domain kwenda kwenye IP Address. Kila mara unapo tembelea tovuti kama tanzaniatech.one DNS inafanya kazi ya kutafsiri domain hiyo kwenda kwenye namba kama hizi 111.230.217.10 na hivyo kunganisha tovuti hiyo na kompyuta yako.

Sasa mara nyingi kampuni zinazo kupa huduma za Internet ndio zinakupa hizi DNS Servers, sasa mara nyingi hizi DNS huwa slow na kufanya speed ya internet yako kuwa slow. Kubadilisha namba hizi kunaweza kufanya speed ya Internet kubadilika kwa haraka sana, ili kubadilisha fuata hatua hapo chini.

Kwenye sehemu ya Kusearch kwenye kompyuta yako, andika Control Panel kisha bofya Enter, kisha chagua Network and Sharing Center.

Baada ya hapo utaona sehemu ya Change Adapter Setting iliyoko kushoto ya pili kutoka chini hapo utaona mitandao mbalimbali ambayo umejiunga nayo, chagua internet unayo tumia kisha chagua Properties.

Baada ya hapo chagua Internet Protocol Setting iliyoko kwenye list hakikisha imewekwa tiki kisha chagua Properties iliyoko chini upande wa kulia kwenye box hilo.

Jinsi ya Kuongeza Speed ya Internet Kwenye Kompyuta

Kwa chini utaona sehemu ya DNS Settings kisha chagua sehemu iliyo andikwa Use the Following DNS server address, Kisha kwenye Prefered DNS Server andika 1.1.1.1 kwa chini yake kwenye Alternate DNS Server andika 1.0.0.1, kisha maliza kwa kubofya OK. Baada ya hapo jaribu utaona Internet yako speed yake imebadilika.

Zima App Zinazotumia Data Bila Kujua

Kuzima app zinazotumia data bila kujua inaweza kusaidia sana kuongeza speed ya internet yako kwani utakuwa unatumia internet kwenye kitu pekee ambacho unafanya kwa wakati huo. Ili kuzima app zinazotumia data unatakiwa kubofya sehemu ya bendera kwenye kompyuta yako kisha chagua Settings.

Baada ya hapo chagua Privacy baada ya hapo upande wa kushoto tafuta sehemu iliyo andikwa Background Apps kisha chagua apps ambazo huziitaji zitumie data kisha bofya kwa kuzima app hizo moja kwa moja.

Jinsi ya Kuongeza Speed ya Internet Kwenye Kompyuta

Zima Peer to Peer Update

Peer to Peer Updates au P2P update hizi ni tofauti na update zile ambazo unazinjua wewe, sehemu hii ikiwa imewashwa inafanya mtu kuweza kutumia Internet ya kompyuta yako bila wewe kujua. Ni muhimu sana sana kuzima sehemu hii.

Ili kuzima sehemu hii bofya sehemu ya Settings kwenye kompyuta yako kisha Chagua Update & Security, kisha bofya Advanced Options kisha shuka mpaka mwisho wa ukurasa huo chini kabisa utaona sehemu imeandikwa Deliver Optimization angalia sehemu iliyo andikwa Allow downloads from other PC’s kisha zima sehemu hiyo.

Jinsi ya Kuongeza Speed ya Internet Kwenye Kompyuta

Tumia Asilimia 100 ya Internet Yako

Maujanja haya ndio ya muhimu zaidi na ndio yanayoweza kuongeza speed ya kompyuta yako kwa asilimia 100. Kifupi ni kwamba Windows inaruhusu kompyuta yako kuweza kutumia asilimia 80 tu ya internet yako, na kama unataka kutumia asilimia zote 100 ni lazima kuwa na uwezo wa kutumia sehemu ya Group Policy.

Sasa kama una Windows 10 au 11 Pro, Windows 10 au 11 Enterprise sehemu hii inapatikana moja kwa moja. Kama unatumia Windows 10 au 11 Home Edition basi ni vyema kufuata hatua kwenye tovuti hii hapa ili kuweza kuwasha sehemu hiyo. Kama unayo moja kati ya windows hizo hapo juu basi endelea kwa kufata hatua zifuatazo.

Kwa kuanza shikilia kitufe cha Bendera kwenye keyboard yako kisha bofya R, baada ya hapo andika maneno haya gpedit.msc kwenye chumba cha Run ukimaliza bofya OK.

Baada ya hapo utaona sehemu ime funguka, kuwa makini sana na sehemu hii kwani ndio inayotumika kuendesha kompyuta yako kwa ujumla.

Upande wa kushoto bofya sehemu iliyoandikwa Computer Configuration baada ya hapo upande wa kulia chini bofya mara mbili sehemu ya  Administrative Template baada ya hapo menu mpya itafunguka kisha chagua kwa kubofya mara mbili sehemu ya Network.

Baada ya hapo chagua QoS Packet Scheduler kisha chagua sehemu ya Limit reservable bandwidth bofya mara mbili kufungua kisha chagua Enabled kisha upande wa kushoto chini utaona sehemu iliyo andikwa Bandwidth limit badilisha na andika namba sifuri 0. Ukimaliza bofya Apply kisha bofya OK kufunga.

Jinsi ya Kuongeza Speed ya Internet Kwenye Kompyuta

Baada ya hapo utakuwa umefanikisha kuongeza speed ya internet kwenye kompyuta yako kwa asilimia 100. Njia hizi ni ngumu kidogo kufuata lakini zitakusaidia sana. Kama una swali lolote unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini.

Jinsi ya Kuongeza Speed ya Internet Kwenye Kompyuta
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kufufua Spika ya Simu Yako Bila Kufungua

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

3 Comments