in

Jiandae na Simu Mpya ya Tecno Camon 17 Pro (Mei 5)

Simi hii ni ya kwanza kwa matoleo ya camon kuwa na kamera ya MP 48

Jiandae na Simu Mpya ya Tecno Camon 17 Pro (Mei 5)

Kampuni ya simu TECNO inayotamba kwa uzalishaji wa simu wa viwango vya hali ya juu na kwa bei rafiki kuzindua rasmi TECNO Camon 17 Pro simu ya kwanza kwa tolea la TECNO CAMON kuja na Selfie Camera ya MP48 na teknolojia ya 4K video resolution kwa kushirikiana na Tigo, Atsoko, DSTV na Coca Cola.

TECNO Camon 17 Pro imekuwa ni gumzo kupitia mitandao ya kijamii kwa muda na kila mtu akionyesha shahuku ya kumiliki kifaa hicho kipya kutoka TECNO. Kampuni ya simu TECNO kupitia mtandao wa kijamii @tecnomobiletanzania imeweka wazi TECNO Camon 17 Pro kuzinduliwa 7/5/2021 ikiambatana na ofa mbalimbali kutoka kwa washirika wake.

Jiandae na Simu Mpya ya Tecno Camon 17 Pro (Mei 5)

TECNO Camon 17pro, simu inayosemekana uwekezaji wake mkubwa upo kwenye Camera kuja kuwa suluhisho kwa Videographers na Photographer katika shughuli zao za upigaji picha na uchukuaji video. Camera ya nyuma ya Camon 17pro ni MP64 ambayo ni bora zaidi wakati wa kuchukua filamu kwa kutumia white and black mode.

Muundo Wa Infinix Zero Ultra 3D Curved Washangaza Wengi

Kampuni ya simu TECNO imekuwa ikiwalenga zaidi vijana kupitia mtiririko wa matoleo mbalimbali kama vile Spark, Pop, Phantom, Pouvoir na Camon zote kubeba applications ambazo ni pendwa kwa vijana.

Kufahamu mengi zaidi kuhusu bidhaa za TECNO tembelea www.tecno-mobile.com

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.