in

TECNO Spark 4 Kupata Android 10 na HiOS 6.2.0

Toleo jipya la Android 10 kwa watumiaji wa simu za Spark 4 (2019)

TECNO Spark 4 Kupata Android 10 na HiOS 6.2.0

Kwa ufupi kabisa, kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanamiliki simu ya TECNO Spark 4 basi habari njema kwako kwani kampuni ya TECNO imetoa sasisho jipya la HiOS 6.2.0 ambalo ni sambamba na mfumo wa Android 10.

Kama unatumia simu hii ya TECNO Spark 4, toleo jipya la Android 10 kwenye simu hii linakuja na mambo mapya kadhaa ikiwa pamoja na

  • Mfumo mpya wa Android 10 pamoja na HiOS 6.2.0
  • Sehemu Mpya ya Dark Mode
  • Sehemu Mpya ya Social Turbo
  • Sehemu mpya ya Game mode

TECNO Spark 4 Kupata Android 10 na HiOS 6.2.0

TECNO Spark 4 Kupata Android 10 na HiOS 6.2.0

Mbali na hayo simu ambazo zinategemewa kupata update hii ni simu za TECNO Spark 4 zenye model namba KC8, kama simu yako ina model namba hiyo basi moja kwa moja unaweza kupata update kupitia Notification, lakini kama ujapata notification unaweza kuangalia update kupitia sehemu ya Settings > System update.

Pia kumbuka sasisho hili linakuja na ukubwa wa GB 1.87 hivyo hakikisha una bando ya kutosha kwenye simu yako, pia hakikisha simu yako imeingia chaji kwa angalau asilimia 70.

Dalili za Ugonjwa wa Kupenda Smartphone Kupita Kiasi

TECNO Spark 4 Kupata Android 10 na HiOS 6.2.0 TECNO Spark 4 Kupata Android 10 na HiOS 6.2.0

TECNO Spark 4 ilizinduliwa mwaka 2019 na simu hii inakuja na kioo cha inch 6.52 kikiwa na resolution ya hadi pixel 720 kwa 1600. Kwa ndani, inakuja na CPU ya quad-core MediaTek Helio A22, sambamba na RAM ya GB 4 huku ikiwa na uhifadhi wa ndani wa hadi GB 64.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.