in

Kwa Nini Usinunue Simu Yenye Umri Zaidi ya Miaka 4

Kwa mwaka huu 2021 usinunue simu iliyotoka mwaka 2017 kurudi nyuma

Kwa Nini Usinunue Simu Yenye Umri Zaidi ya Miaka 4

Kwa sasa ni wazi kuwa kila kampuni ya simu inajitahidi kwenda na wakati kwa kuzindua simu mpya zenye sifa mbalimbali na zinazo endana na wakati.

Lakini kama wewe ni kama mimi ni wazi kuwa kuna wakati unataka kununua simu ya bei rahisi na hivyo unajikuta unataka kununua simu ya miaka ya nyuma kwa sababu mara nyingi simu hizi huwa zinapatikana kwa bei nafuu zaidi kuliko simu za mwaka husika.

Lakini kabla ya kufanya hivyo pengine unipe muda wako nikwambie ni kwanini usinunue simu yenye umri zaidi ya miaka 4 kuanzia simu hiyo ilipo zinduliwa rasmi. Hii ni sawa na kusema kwa sasa mwaka 2020 usinunue simu iliyo zinduliwa kuanzia mwaka 2017 kurudi nyuma.

Basi bila kupoteza muda moja kwa moja twende kwenye sababu hizi ambazo na uhakika zinaweza kusaidia kufanya maamuzi bora ya simu ya mwaka gani ambayo unastahili kununua.

Mfumo wa Uendeshaji

Kwa Nini Usinunue Simu Yenye Umri Zaidi ya Miaka 4

Mwaka 2017, kampuni ya Google ilizindua mfumo wa Android 8.0 na baadae 8.1 mfumo huu wa Android kwa sasa unatumika kwenye simu nyingi sana lakini wakati sasa tukiwa tunaelekea kwenye mfumo wa Android 12 ni wazi kuwa mambo mengi sana yanategemewa kubadilika hii ikiwa pamoja na apps ambazo zitakuwa zinatumika kwenye mfumo huo.

Kama unatumia simu ya mwaka 2017 ni wazi kuwa utakosa mengi sana kwenye apps mbalimbali za Android hii ni kwa sababu Google ulazimasha watengenezaji wa apps kutengeneza apps kwa kuzingatia mfumo mpya wa Android ambao kwa sasa ni Android 11 ambayo ni API Level 30. Bila kufanya hivyo watengenezaji wa apps hushindwa kuweka apps hizo kwenye soko la Play Store.

Hivyo basi kwa kutumia simu ya mwaka 2017 kurudi nyuma ni wazi kuwa watengenezaji wa app hawatengenezi apps kulingana na mfumo wa simu yako hivyo ni wazi kuwa kuna baadhi ya apps ambazo zitashindwa kufanya kazi vizuri kwenye simu yako ya Android, hasa yenye mfumo wa Android 8 kurudi nyuma.

Uwezo wa Battery

Kwa Nini Usinunue Simu Yenye Umri Zaidi ya Miaka 4

Ni wazi kuwa Battery zote huwa na muda maalum wa kudumu na chaji, kwa mujibu wa tovuti ya charbycharge, baadhi ya battery za simu huwa na uwezo wa kudumu na chaji vizuri kwa muda wa miaka 2 au 3 na baadae kupungua uwezo kwa hadi asilimia 20.

Hivyo basi hii ni sawa na kusema kuwa mara nyingi simu za mwaka 2017 kurudi nyuma huwa na uwezo mdogo wa kudumu na chaji, hii ni kwasababu mara nyingi watumiaji wa simu za miaka ya nyuma hupendelea kununua simu hizi kutoka kwa watu au simu ambazo zimetumika nje ya nchi.

Uwezo wa Simu

Kwa Nini Usinunue Simu Yenye Umri Zaidi ya Miaka 4

Kama ulikuwa hujui, mara nyingi simu zenye umri mkubwa huwa na uwezo mdogo wa processor kuliko simu zilizo zinduliwa mwaka usika. Zipo sababu nyingi kwanini simu za zamani huwa slow kuliko simu za mwaka usika.

Moja ya sababu kubwa ni kuwa processor zinazo tengenezwa miaka ya nyuma kwa mfano mwaka 2017 na kurudi nyuma huwa zina angalia zaidi uwezo wa apps zinazolenga mfumo wa Android 8 na kurudi nyuma. Lakini pale mfumo huu unapo pitwa na wakati apps nyingi hushindwa kufanya kazi kwenye simu za mwaka 2017 kutokana na processor hizo kuwa na uwezo mdogo kuliko app husika.

Pia kumbuka watengenezaji wa apps huangalia zaidi mfumo mpya wa Android na kuhakikisha apps zao zinafanya kazi vizuri zaidi kwenye simu zenye mfumo mpya wa Android na sio kwenye simu zenye mfumo wa Android wenye umri zaidi ya miaka 4.

Pia imeshawahi kuripotiwa kuwa baadhi ya kampuni hufanya simu za zamani kuwa slow baada ya miaka kadhaa ili kusudi wateja wake waendelee kununua simu mpya zinazotoka kila mwaka.

Sababu Nyingine

Sidhani kama kuna sababu nyingine kubwa kama hizo hapo juu, kwa sababu kama simu ikisha pungua uwezo wa battery kwa asilimia 20, na kushindwa kuinstall baadhi ya apps, bila kusahau kupungua uwezo wake wa processor na hivyo kuwa slow sidhani kama simu hii inakufaa kwa matumizi.

Lakini kwa kuongezea hizi ni baadhi ya sababu nyingine kwanini usinunua simu za zamani zaidi ya miaka 4, kama unasoma post hii mwaka huu 2021 basi usinunue simu za mwaka 2017 kurudi nyuma.

  • Kushinda kupata mfumo mpya wa Android kwa sababu mara nyingi simu hizo hupewa mwaka mmoja au miwili ya update na baada ya hapo simu hizo kuachwa.
  • Simu kupata moto mara kwa mara.
  • Kushindwa kufungua baadhi ya games na apps mpya.

Na hizo ndio baadhi ya sababu ambazo ni kwanini usinunue simu zenye zaidi ya umri wa miaka 4 kuanzia ilipo zinduliwa. Kwa sasa kama unasoma makala hii mwaka 2021, basi unatakiwa kujua kuwa usinunue simu inayo anzia mwaka 2017 kurudi nyuma.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.