in

Jinsi ya Kutuma na Kupokea SMS kwa Kutumia Kompyuta

Jifunze njia ya kukusaidia kutumia kompyuta kutuma SMS

Jinsi ya Kutuma na Kupokea SMS kwa Kutumia Kompyuta

Habari na karibu kwenye maujanja, leo tutaenda kuangalia njia mpya ya kukusaidia kutumia na kupokea ujumbe mfupi au SMS kwa kutumia kompyuta yako. Zipo sababu nyingi zinazoweza kukufanya uhitaji kutuma na kupokea ujumbe mfupi kwa kutumia kompyuta, moja ya sababu hizo ni pale unapokuwa unafanya kazi kwenye kompyuta yako.

Ukweli ni kuwa ni ngumu sana kutumia vifaa viwili kwa wakati mmoja tena hasa pale unapokuwa kwenye mazingira ya kazi, vilevile ofisi nyingi hapa Tanzania hazipendi tabia ya kushika simu huku unafanya kazi, sasa kama wewe umekuwa ukipata shida ya namna hii njia hii itakusaidia na utaweza kutumia simu yako kwenye sehemu ya SMS kwa kupitia kompyuta yako.

Njia hii haitaji uwe na ujuzi wowote bali inakuitaji tu uwe unatumia kisakuzi au Browser ya Google Chrome, vilevile unatakiwa kuwa na simu yako Android na bila kusahau kompyuta yako ya mfumo wowote wa Windows PC au hata Mac PC. Kama una mambo yote haya unaweza kuendelea kwa hatua zifuatazo.

Tovuti za Kujifunza Kutengeneza Apps na Website Bure 100%

Kwanza chukua simu yako ya Android kisha pakua App ya MightyText hapo chini na install vizuri kwenye simu yako. Baada ya kuinstall ingia kwenye kompyuta yako kisha install extensions ya MightyText ambayo nayo pia inaptikana hapo chini, kisha baada ya hapo endelea kwa kufuatilia maelekezo marahisi kwenye video hapo chini.

Download App Hapa

Download Extension Hapa

Baada ya kumaliza njia hizo zote na ukakika utakuwa umeweza kutuma na kupokea meseji kwa kutumia kompyuta yako. Basi kama kuna mahali umekwama au kama una maoni, ushauri au mashwali unaweza kutuandikia hapo chini kwenye sehemu ya maoni, Mpaka siku nyingine endelea kutembelea Tanzania Tech Byee!.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment