Jinsi ya Kuhamisha Chats za WhatsApp Kwenda Telegram

Jinsi ya kuhamisha chats zako zote kutoka WhatsApp kwenda Telegram
Jinsi ya Kuhamisha Chats za WhatsApp Kwenda Telegram Jinsi ya Kuhamisha Chats za WhatsApp Kwenda Telegram

Hivi karibuni WhatsApp ilitangaza kubadilisha vigezo na masharti ya utumiaji wa programu yake, ikiwa pamoja na sera mpya za faragha ambazo zilikuwa zianze kutumika mwezi huu wa pili.

Sheria hizo zilikuwa zinawataka watumiaji kukubaliana na sera mpya za faragha kuwa baadhi ya data za watumiaji zitatumwa kwa kampuni mama ya programu hiyo ambayo ni Facebook. Kupitia Facebook data hizo zinaweza kuendelea kutumika zaidi kwaajii ya kuboresha programu hiyo na kwaajili ya kibiashara.

Baadhi ya data zitakuwa zinachukuliwa na Facebook ni pamoja na model namba ya simu yako, mfumo wa uendeshaji, kiasi cha battery ya simu yako, Uwezo wa mtandao wa simu, Majira ya saa, Namba za utambulisho za simu yako, Jinsi unavyotumia WhatsApp, Status Update zako, Sehemu ya Kuhusu wewe, Profile Picture au DP na mengine mengi.

Advertisement

Jinsi ya Kuhamisha Chats za WhatsApp Kwenda Telegram

Mabadiliko hayo hayakuwa marahisi kwani yamepelekea watumiaji wengi wa WhatsApp kuhama kutoka mtandao huo kwa kuhofia usalama wa programu hiyo na kuhamia kwenye mitandao ya Signal na Telegram.

Kupitia makala hii nitakuonyesha njia rahisi ambayo unaweza kutumia kuhamisha meseji au chats zako kutoka WhatsApp kwenda Telegram. Njia hii ni rahisi na unaweza kufanya kwenye simu zote za Android kwenda iOS.

Amisha Chats Kutoka WhatsApp kwende Telegram

Kwa kuanza unatakiwa kujua kuwa unaweza kuhamisha chats moja moja za WhatsApp na sio chats nyingi kwa wakati mmoja. Mpaka sasa bado hakuna njia ya kuhamisha chats zote kwa pamoja kwenda Telegram.

Fungua programu ya WhatsApp kisha fungua meseji ambazo unataka kuhamisha kwenda Telegram, pia unaweza kuhamisha meseji za group pia. Baada ya kufungua chat bofya vitufe vitatu ndani ya chati.

Jinsi ya Kuhamisha Chats za WhatsApp Kwenda Telegram

Baada ya hapo kwenye Menu hiyo chagua sehemu ya More, iliyopo chini mwisho kabisa baada ya kubofya vitufe vitatu.

Jinsi ya Kuhamisha Chats za WhatsApp Kwenda Telegram

Baada ya hapo endelea kwa kuchagua sehemu ya Export chat inayotokea kwenye Menu baada ya kubofya sehemu ya More.

Jinsi ya Kuhamisha Chats za WhatsApp Kwenda Telegram

Baada ya hapo chagua kama unataka kuhamisha chats au meseji zako bila media au pamoja na media, ukichagua Include Media utapata chats au meseji zako zote zikiwa na picha na kila kitu, lakini ukichagua Without Media utaweza kupata chats au meseji pekee bila picha.

Jinsi ya Kuhamisha Chats za WhatsApp Kwenda Telegram

Baada ya hapo moja kwa moja itafunguka sehemu ya Share mara baada ya kuchagua menu ya Include Media au Without Media. Moja kwa moja chagua Telegram kwenye list ya app kwenye sehemu ya Share.

Jinsi ya Kuhamisha Chats za WhatsApp Kwenda Telegram

Baada ya hapo kama moja kwa moja utaweza kuchagua namba ya mtu ambaye yupo kwenye telegram, kama ni group moja kwa moja tengeneza group jipya kwa kubofya sehemu ya Create a new group to import.

Kama group kama hilo lipo kwenye telegram utaletewa kwa chini ukiwa na uwezo wa kuweka meseji zote kwenye group hilo, kwa kufanya hivyo hauta poteza meseji zako zilizopo kwenye group kwa muda huo.

Jinsi ya Kuhamisha Chats za WhatsApp Kwenda Telegram

Baada ya hapo moja kwa moja utaweza kuanza kuona chat au meseji zako zikiwekwa kwenye mtandao wa telegram, hakikisha unasubiri hadi itakapo fika 100.

Jinsi ya Kuhamisha Chats za WhatsApp Kwenda Telegram

Baada ya hapo moja kwa moja utaweza kuona meseji zako kwenye app ya telegram bila kupoteza kitu chochote. Njia hii inafanya kazi kwenye programu zote za WhatsApp na WhatsApp Bussines, kitu cha muhimu ni kuhakikisha unayo namba ya mtu husika kwenye programu zote za WhatsApp na Telegram.

Kwa kufuata hatua hizo natumani utakuwa umeweza kuhamisha chats zako au meseji zako kutoka WhatsApp kwenda Telegram. Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kuhamisha chats kutoka WhatsApp kwenye mfumo wa Android kwenda iOS. Kuendelea kujifunza zaidi endelea kutembelea Tanzania tech kila siku.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use