in

Jinsi ya Kupata Internet Sehemu Isiyo na Network (Hasa Vijijini)

Hizi hapa njia za kusaidia kupata network sehemu zenye network hafifu

Jinsi ya Kupata Internet Sehemu Isiyo na Network (Hasa Vijijini)

Kipindi hichi cha sikukuu watu wengi usafiri kwenda sehemu mbalimbali ambazo nyingi zinakuwa na shida ya network au mtandao, hii hufanya watu wengi kushindwa kuwasiliana au kukosa internet pale tu wanapokuwa sehemu hizo ambazo minara ya mawasiliano inakuwa mbali.

Kupitia makala hii nitaenda kukwambia njia kadhaa ambazo zinaweza kukusaidia kupata mawasiliano ya simu au internet hasa unapokuwa kwenye sehemu ambazo hazina Network.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kumbuka njia hizi zinaweza kusaidia hasa kama eneo ulilopo lina uwezekano wa kupata mtandao lakini simu yako ndio haipati network, Njia hizi haziwezi kufanya kazi kama eneo ulilopo halina network kabisa hivyo ni vyema kuhakikisha umepata network angalau kidogo kabla ya kufanya njia hizi. Baada ya kusema hayo basi twende tukangalie njia hizi.

Washa Data Roaming

Jinsi ya Kupata Internet Sehemu Isiyo na Network (Hasa Vijijini)

Kama unataka kutumia Internet na eneo ulipo hakuna internet vizuri basi unaweza kujaribu kuwasha Data Roaming, sehemu hii ambayo inapatikana kwenye kila smartphone inakuruhusu kutumia network ya mtandao ulipo jirani na wewe bila kujali kama ni network ya mtandao wa simu unao tumia.

Hivyo basi, haijalishi unatumia Vodacom, Tigo, au Airtel sehemu hii ya Data roaming itakusaidia kuunganisha Internet kwenye mnara wa mtandao uliopo karibu na wewe. Kumbuka sehemu hii inaweza kufanya bando kuisha haraka zaidi.

Tumia Open Signal

Jinsi ya Kupata Internet Sehemu Isiyo na Network (Hasa Vijijini)

Open Signal ni app inayopatikana kwa watumiaji wa simu za Android, uzuri wa app hii ni kuwa inaweza kukusaidia sana kujua mahali ambapo network inapatikana zaidi kwenye eneo ulilopo.

App hii ina uwezo mkubwa wa kujua mahali minara ya mtandao unaotumia inapo patikana na pia ina kuja na ramani pamoja na dira ambayo inaonyesha muelekeo ili kujua minara hiyo inapo patikana. Unaweza kupata app hii kupitia link hapo chini.

Washa na Kuzima Airplane Mode

Jinsi ya Kupata Internet Sehemu Isiyo na Network (Hasa Vijijini)

Kama kwa namna moja ama nyingine upo kwenye eneo ambalo lina aina moja ya mtandao kwa mfano 2G ambayo mara nyingi huandika E basi unaweza kutumia njia hii ya kuwasha na kuzima sehemu ya Airplane Mode na utaweza kuna Network imebadilika.

Kitu cha muhimu hakikisha una subiri angalau sikunde Tano baada ya kuwasha sehemu hiyo, kwani kwa kufanya hivyo unaruhusu simu yako kushika mawimbi kwenye mnara uliopo karibu na wewe.

Restart Simu Yako

Jinsi ya Kupata Internet Sehemu Isiyo na Network (Hasa Vijijini)

Mbali na faida nyingi zinazopatikana pale unapo restart simu yako angalau mara moja kwa siku, pia kurestart simu yako kunaweza kusaidia sana pale unapo ona unakosa mawasiliano kutokana na kuwepo kwenye eneo ambalo halina Network vizuri.

Njia hii ni nzuri sana hasa pale unapo jaribu njia iliyopita ya kuweka Airplane Mode na ukaona haija saidia.

Mengine Yanayoweza Kusaidia

Pamoja na mambo yote hayo hapo juu, unaweza kufanya mambo mengine madogo madogo ambayo yanaweza kusaidia kupata Network kwa haraka na kwa urahisi. Mambo hayo ni

  • Hakikisha simu yako inachaji ya kutosha – Kama simu yako ina chaji kidogo inaweza kuwa ni moja kati ya sababu zinazofanya ukose mtandao vizuri.
  • Funga programu ambazo hazitumiki – Mara nyingi kama simu yako inayo programu nyingi  zinatumia network kwa pamoja huwa ni chanzo cha simu yako kukosa network vizuri, hivyo hakikisha unafunga programu zote kisha tumia programu moja baada ya nyingine hasa unapokuwa kwenye eneo ambalo halina network vizuri.
  • Shika simu yako vizuri – Simu nyingi za sasa zinakuja na antenna kwa nyuma, antenna hiyo inakuwa karibia na sehemu ya chini au ya juu ya simu hivyo unaposhika simu yako hakikisha unashika simu yako vizuri na usizibe kwa nguvu eneo la nyuma la simu yako.
  • Hakikisha simu yako inalo toleo jipya la mfumo wa Uendeshaji (OS) – Unaweza kudhani hii sio sababu lakini kama simu yako inayo update basi hakikisha una update kabla ya kwenda kwenye sehemu yenye shida ya mtandao kwani pamoja na sababu nyingine hii inaweza kuwa sababu ya simu yako kukosa network.

Na hayo ndio baadhi ya mambo ambayo unaweza kufanya ili kuweza kupata Network sehemu ambayo haina network ya kutosha.

Kumbuka ni muhimu sana kujua kuwa njia hizi zinafanya kazi kwenye maeneo ambayo yana mtandao kidogo na sio kwenye maeneo ambayo hayana mtandao kabisa.

Natumaini kwa kufanya njia hizi utaweza kupata mtandao hasa unapokua kijijini kwenu kipindi hichi cha sikukuu.. Kama una swali au maoni basi unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini. Mpaka makala nyingine napenda kukutakia heri ya sikukuu ya Christmas ?.

Jinsi ya Kupata Internet Sehemu Isiyo na Network (Hasa Vijijini)
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Jinsi ya Kupata File Lolote kwa Haraka (MP3,MP4,ZIP,PDF,ISO)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment