in

Jinsi ya Kutoa Pesa Kutoka Paypal Ukiwa Tanzania (Tigo & Bank)

Utaweza kutoa pesa kuja kwenye mobile money au akaunti yako ya benki

Jinsi ya Kutoa Pesa Kutoka Paypal Ukiwa Tanzania (Tigo & Bank)7:18

Ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye amewahi kupokea pesa kutoka nje ya nchi alafu asitamani kutumia Paypal, lakini kwa masikitiko makubwa kwa hapa Tanzania hakuna njia ya kutoa pesa kutoka paypal kuja bank hadi sasa.

Kabla ya kuanza ni vyema ujue kuwa ni muhimu kuwa muangalifu na pesa zako na kuhakiksha kuwa unafuata vigezo na masharti yote ya huduma unayo tumia.

Pia kumbuka njia hii haiku tengenezwa maalum kwa kutuma pesa zako mwenye ukiwa sehemu moja bali njia hii imetengenezwa kusaidia watu kutoka nje ya nchi kutuma pesa kutoka paypal kwenda kwenye akaunti ya bank au mobile money ya mtu aliyopo hapa Tanzania.

Unaweza kutumia njia hii kujitumia pesa mwenyewe lakini kumbuka hiyo ni kinyuma na vigezo na masharti ya huduma hii. Hakikisha unakua makini unapotumia njia hii na pia unaweza kutuma kiasi kidogo kuona kama njia hii inafanya kazi kwa asilimia 100.

Tembelea Tovuti ya Xoom Hapa

Kuonyesha kwamba njia hii inafanya kazi na imethibitishwa na kampuni za simu kama vile Tigo unaweza kuona meseji nilizotumiwa mwezi wa pili mwaka 2021 ambapo Tigo walionyesha kutangaza kutumia njia hii kutuma pesa kupitia kwa ndugu na jamaa kupitia Xoom.

Ongeza Ukubwa wa Maandishi Kwenye Apps Zote (Android)

Jinsi ya Kutoa Pesa Kutoka Paypal Ukiwa Tanzania (Tigo & Bank)

Kwa maujanja zaidi hakikisha unaendelea kutembelea tovuti ya Tanzania tech, pia hakikisha unajiunga nasi kupitia channel yetu kupitia mtandao wa YouTube. Kama unataka kujifunza zaidi unaweza kusoma hapa kujua jinsi ya kupokea pesa kutoka nje ya nchi kuja kwenye namba yako ya simu ya mobile money.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.