in

Apple Yazindua Simu Mpya za iPhone 12 na 12 Pro

Sifa na bei za iPhone 12 mini, iPhone 12, iPhone 12 Pro na iPhone 12 Pro Max

Apple Yazindua Simu Mpya za iPhone 12 na 12 Pro

Kampuni ya Apple hapo jana ilifanikiwa kuzindua simu matoleo mpya ya simu zake mpya za iPhone 12, simu ambazo zinakua kwa matoleo manne tofauti yaani iPhone 12 mini, iPhone 12, iPhone 12 Pro pamoja na iPhone 12 Pro Max.

Sifa za iPhone 12 Mini

Tukianza na iPhone 12 Mini ambayo ndio simu ndogo kwa size kuliko zote kwenye matoleo haya, simu hii inakuja na kioo cha inch 5.4 kilicho tengenezwa kwa teknolojia ya Super Retina XDR OLED display. Kioo hicho kinakuja na uwezo wa resolution ya hadi pixel 1080 kwa 2340.

Mbali na hayo, kioo hicho pia kimeongezewa ubora na ugumu kwa kutumia teknolojia mpya ya oleophobic coating ambapo kioo hicho hakipati michubuko kwa urahisi (Scratch-resistant) au kuvunjika kwa urahisi pale simu hiyo itakapo anguka.

Apple Yazindua Simu Mpya za iPhone 12 na 12 Pro

Tukiwa bado kwa mbele, iPhone 12 Mini inakuja na kamera mbili kwa mbele, kamera kuu ikiwa na Megapixel 12 huku kamera ya pili ikiwa ni SL 3D, (depth/biometrics sensor).

Kwa nyuma simu hii inakuja na kamera mbili za Megapixel 12 kila moja huku kamera hizo zikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K. Mbali na hayo, kamera za iPhone 12 mini pia zina kuja na teknolojia ya HDR, pamoja na Flash ya Quad-LED dual-tone.

Kwa upande wa sifa za ndani za iPhone 12 mini inakuja na processor ya Apple A14 Bionic (5 nanometer) inayo saidiwa na CPU yenye uwezo wa hadi Hexa-core. CPU hiyo inapewa nguvu na RAM ambayo bado haijajulikana pamoja na uhifadhi wa ndani wa kuchagua kati ya GB 64, GB 128, na GB 256. iPhone 12 mini haina sehemu ya kuchomeka memory card hivyo huwezi kuongeza uhifadhi wa ndani.

Sifa za iPhone 12

Tukiamia kwa upande wa iPhone 12, simu hii inakuja na kioo cha inch 6.1 kioo kilicho tengenezwa kwa teknolojia ile ile ya Super Retina XDR OLED display, lakini tofauti na iPhone 12 mini simu hii inakuja na resolution ya hadi pixel 1170 kwa 2532.

Kioo hicho pia kinakuja na teknolojia inayo fanana na iPhone 12 mini ambapo kioo hicho sasa kimeongezewa ubora na ugumu kwa kutumia teknolojia mpya ya oleophobic coating, teknolojia ambayo hufanya kioo hicho kuwa kigumu zaidi.

Kwa upande wa kamera za selfie, zinafanana kabisa kwani iPhone 12 inakuja na kamera mbili kwa mbele, kamera kuu ikiwa na megapixel 12 na nyingine ikiwa ni SL 3D, (depth/biometrics sensor).

Kwa nyuma pia, iPhone 12 na iPhone 12 mini zinakuja na sifa zinazofanana kwa kuwa na kamera mbili zenye Megapixel 12 kila moja huku kamera hizo zikiwa na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K.

Kwa upande wa sifa za ndani za iPhone 12 inafanana kabisa na iPhone 12 mini kwani inakuja sifa zilezile zinazopatikana kwenye 12 mini.

Tofauti ya iPhone 12 mini na iPhone 12

Sifa za iPhone 12 Pro

Kwa upande wa iPhone 12 Pro, sifa ni zilezile zinazofanana na iPhone 12 tofauti iliyopo kwenye simu hii na iPhone 12 ni pamoja na idadi ya kamera za nyuma ambapo iPhone 12 Pro inakuja na kamera nne kwa nyuma ambapo kamera tatu zinakuja na uwezo wa Megapixel 12 kila moja na nyingine moja ni TOF 3D LiDAR scanner (depth).

Tofauti nyingine kati ya iPhone 12 na iPhone 12 Pro ni pamoja na uhifadhi wa ndani kwani iPhone 12 pro ina anza kupatikana kuanzia GB 128, GB 256, pamoja na GB 512. Mbali na hayo sifa nyingine zinafanana kabisa na iPhone 12.

Sifa za iPhone 12 Pro Max

Tukiamia kwenye toleo la mwisho la iPhone 12 Pro Max, sifa ni zilezile zinazofanana na iPhone 12 Pro tofauti iliyopo kwenye iPhone 12 Pro Max na iPhone 12 Pro ni pamoja na Kioo cha iPhone 12 Pro Maxi ni kikubwa zaidi kwani kina kuja na ukubwa wa nchi 6.7 huku kikiwa na resolution ya hadi pixel 1284 kwa 2778.

Mbali na hayo sifa nyingine zote zina fanana kati ya iPhone 12 Pro na iPhone 12 Pro Max. Kwa upande wa battery bado haija julikana uwezo halisi wa battery hizo hivyo ni wazi simu hizo zote zitakuwa zina tofautina kwenye uwezo wa kudumu na chaji kulingana na matumizi yako.

Tofauti ya iPhone 12 Pro na iPhone 12 Pro Max

Mbali ya simu hizo pia kampuni ya Apple imetangaza ujio wa teknolojia mpya kwenye simu zake, kama vile teknolojia ya 5G kwenye simu zote za iPhone 12, pamoja na teknolojia ya SafeMag ambayo inaruhusu mtumiaji kunatisha chaja na vitu vingine mbalimbali nyuma ya simu hizo ikiwa pamoja na pochi maalum ambayo inaweza kutumika kuweka kadi za benki na vitu vingine mbalimbali.

Apple Yazindua Simu Mpya za iPhone 12 na 12 Pro

Kwa upande wa bei simu hizi zinategemewa kupataikana hivi karibuni, huku iPhone 12 na iPhone 12 Pro ikitegemewa kuanza kupatikana kuanzia October 16 na iPhone 12 mini na iPhone 12 Pro Max zikitegemewa kupatikana kuanzia Novemba 13. Kwa Tanzania unaweza kusoma bei ya simu hizi kupitia hapo chini.

Kumbuka bei zote ni makadirio hivyo bei hizo zinaweza kubadilika pale simu hizo zitakapo patikana hapa Tanzania. Kumbuka bei inabadilika kulingana na masoko.

Apple Yazindua Simu Mpya za iPhone 12 na 12 Pro
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Zifahamu Hizi Hapa Bei za Simu Mpya za Redmi Note 13

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.