in

Instagram Yasherekea Miaka 10 kwa Maujanja Haya

Instagram imeficha zawadi kwa ajili ya watumiaji wote wa mtandao huo

Instagram Yasherekea Miaka 10 kwa Maujanja Haya

Miaka 10 iliyopita tarehe 6 October mtandao maarufu wa Instagram ulizaliwa rasmi, hiyo inafanya mwaka huu 2020, Instagram kusherekea miaka 10 ya kuunganisha watu na biashara mbalimbali kote duniani.

Katika kusherekea miaka hiyo 10, kwa mwezi huu October instagram imekuja na maujanja yaliyojificha ambapo unaweza kubadilisha Icon ya Instagram kupitia ndani ya app hiyo moja kwa moja. Unaweza kuchagua Icon mbalimbali ikiwa pamoja na Icon zilizotumika kwenye mtandao huo kwenye miaka ya mwanzoni wakati mtandao huo ulipo zaliwa kwa mara ya kwanza.

Unaweza kuangalia video hapo chini ili kujua jinsi ya kubadilisha Icon kwenye app yako ya Instagram kwa urahisi na haraka.

Unaweza kufanya njia hizi kupitia simu yako ya mfumo wa Android lakini pia unaweza kufanya kupitia mfumo wa iOS. Thats it! kujua maujanja mengine unaweza kuhakikisha unajiunga nasi kupitia channel yetu ya Tanzania Tech kupitia mtandao wa YouTube.

Tengeneza Video za Mitandao ya Kijamii Bila Kuwa na Ujuzi

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.