TikTok na WeChat Kufungiwa Kwenye Masoko ya App Marekani

Watumiaji wa marekani hawatoweza kupakua app hiyo kupitia app store zote
TikTok na WeChat Kufungiwa Kwenye Masoko ya App Marekani TikTok na WeChat Kufungiwa Kwenye Masoko ya App Marekani

Idara ya Biashara ya Marekani imetangaza kuwa itapiga marufuku programu za TikTok na WeChat kwenye masoko ya Apps (Play Store na App Store) kuanzia siku ya Jumapili hii. Kwa sasa, TikTok haitaathiriwa sana na sheria hii kwani ikiwa mtumiaji tayari anayo app hiyo anaweza kuendelea kutumia app hiyo kama kawada, lakini hawatoweza ku-update app hiyo kwa namna yoyote.

Aidha kwa upande wa WeChat inakabiliwa na vizuizi vikali zaidi, kwani sheria hiyo mpya itafanya iwe kinyume cha sheria kutumia mtandao wa WeChat ikiwa pamoja na kuhamisha data zozote ukiwa nchini marekani, data hizo ni pamoja na kutuma meseji, picha, pamoja na kutumia njia za malipo zilizopo ndani ya app hiyo.

Sheria hizo za kuzuia uhamishaji wa data, zitatumika pia kwa mtandao wa TikTok kuanzia Novemba 12 ikiwa mmiliki wake ByteDance hajafikia makubaliano ya kuuza shughuli zake za Marekani kwa kampuni ya Marekani.

Advertisement

Hivi karibuni ilisemekana kuwa kampuni ya Oracle ilifikia makubaliano na kampuni ya TikTok, lakini siku chache zilizopita kituo cha runinga cha kiingereza kinacho milikiwa na china (CGTN) kiliripoti kuwa ByteDance haitauza mtandao huo kwa kampuni ya Marekani.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Ikulu ya White House, inasemekana kwamba Rais Trump amekataa masharti ya mpango wa kampuni ya Oracle na ByteDance na ana mpango wa kuizuia makubaliano hayo hivi karibuni.

“Vitendo vya leo vinathibitisha tena kuwa Rais Trump atafanya kila kitu kwa uwezo wake kuhakikisha usalama wetu wa kitaifa na kuwalinda Wamarekani kutokana na vitisho vya Vyama vya Kikomunisti vya China,” alisema Katibu wa Idara ya Biashara ya Marekani Wilbur Ross.

“Kwa maagizo ya Rais, tumechukua hatua kubwa kupambana na mkusanyiko mbaya wa data za wamarekani unaofanywa na Uchina.” aliongeza Wilbur Ross.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use