in

Hizi Hapa Apps Muhimu kwaajili ya Mwezi wa Ramadhani

Tanzania Tech tunakutakia “Mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan”

App-nzuri-za-Ramadhan

Kila mwaka Waislamu wote duniani ujumuika pamoja na kufunga kila ifikapo mwezi mtukufu wa Ramadhan, mwezi huo waumini wote wa dini ya kiislamu hufanya Sala pamoja na mambo mengine mazuri ya kumpendeza Mungu ikiwa kama ni sehemu ya ibada ya mwezi huo. Kwa sasa tupo kwenye siku za mwanzo za kipindi hicho cha mwezi mtukufu wa Ramadhan, Tanzania Tech tunaungana na watanzania wote kuwatakia Waislamu wote “Mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan”.

Kwa upande wa Teknolojia, zipo njia mbalimbali za kukusaidia kuendelea kufurahia teknolojia huku unaendelea na funga yako kwenye mwezi huu mtukufu. Tanzania Tech tumekuandalia App nzuri za kukusaidia kwenye mwezi huu wa Ramadhan, na bila kupoteza muda basi twende tukaangalia App hizo nzuri.

Muslim Pro – Ramadan 2020

Muslim Pro ni Moja kati ya App muhimu kwa Muislamu yoyote, App hii inakupa uwezo wa kujua muda wa sala, unaweza kusoma vitabu vya mungu pamoja na njia za kuweza kuboresha funga yako hasa kwenye mwezi huu mtukufu wa Ramadhan. App hii ni bora sana na kama huna app hii nakushauri download app hii sasa.

Jaribu App Mpya ya Tanzania Tech Lite

Quran Majeed – Ramadan 2020 قرآن‎

Hii ni App nyingine nzuri sana kwa mwezi huu mtukufu, app hii itakupa uwezo wa kusikiliza Quran kwa haraka. Mbali na hayo unaweza kuhifadhi Aya fulani kwa haraka na kwa urahisi.

Muslim Dua Now – Dua & Azkar

Hii ni app nyingine nzuri sana kuwa nayo kama wewe ni Muislam, App hii itakupa uwezo wa kupata Dua mbalimbali kwa ajili ya vitu mbalimbali au matukio mbalimbali. App hii itakupa Dua tofauti ambazo unaweza kutumia pale unapokuwa na uhitaji.

Ramadan 2020

Hii ni App nyingine nzuri sana kwa mwezi huu, App hii itakupa uwezo wa kujua muda wa Dua pamoja na sala mbalimbali za mwezi huu pamoja na mambo mengine mengi.

Islamic Calendar – Ramadan, Quran, Qibla, Dua

App hii ni app nyingine nzuri sana kwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhan, App hii itakupa uwezo wa kufanya maombi kwa muda sahihi ikiwa pamoja na muda wa Athan pamoja na mambo mengine mbalimbali.

Apps za Kurahisisha Matumizi ya Mtandao wa Instagram

Na hizo ndio App nilizo kuandalia kwa siku ya leo, kama una maoni au maswali au kuna app nyingine ambazo unazijua ni nzuri zaidi kwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhan tuambie kwenye sehemu ya maoni hapo chochote. Kama ulipitwa na App nyingine nzuri za Android unaweza kusoma hapa.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Avatar

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

3 Comments