Samsung Yatangaza Ujio wa External Mpya Zenye Fingerprint

External hii inakuja na uwezo wa kuweka alama za vidole za watu zaidi ya watatu
Samsung Yatangaza Ujio wa External Mpya Zenye Fingerprint Samsung Yatangaza Ujio wa External Mpya Zenye Fingerprint

Wakati kampuni nyingine zikiwa zinapambana kuja na external zenye uhifadhi mkubwa, Kampuni ya Samsung hivi karibuni imeonyesha ubunifu wa aina yake kwa kuja na external yenye ulinzi wa alama za vidole (Fingerprint).

Samsung Yatangaza Ujio wa External Mpya Zenye Fingerprint

Kwa mujibu wa Samsung, External hizo ambazo zimepewa jina la T7 Touch external SSD zinakuja kwa size tofauti kuanzia GB 500 hadi TB 2. Mbali na ukubwa wake wa uhifadhi external hizi pia zinakuja zikiwa zimetengezwa na material ya solid aluminum, material ambayo kwa mujibu wa Samsung yanasaidia external hizi kuto kuharibika hasa pale zinapo anguka kuanzia umbali wa kama futi sita na nusu au pungufu.

Advertisement

Kingine ambacho ni bora kwenye T7 Touch external SSD ni kuwa inakuja ikiwa na SSD bora zaidi yenye speed hadi kufikia MB 1,000 kwa sekunde ikiwa unatuma kitu ndani ya SSD hiyo, na speed ya hadi MB 1,050 kwa sekunde ikiwa unaotoa kitu ndani ya SSD hiyo.

https://youtu.be/K8QF7dnpxTY

Kama unavyoweza kuona kwenye video hapo juu, sehemu ya ulinzi ya fingerprint kwenye external hiyo ya T7 Touch inafanya kazi bila kutegemea kama kifaa unachotumia kina sehemu hiyo ama lah..!. T7 Touch inaruhusu kuhifadhi hadi alama za vidole za watu wanne tofauti, ili kuruhusu kutumia external hiyo na ndugu na jamaa nyumbani, shuleni au hata kwenye maeneo ya kazi.

Samsung Yatangaza Ujio wa External Mpya Zenye Fingerprint

External hiyo ya T7 Touch, inategemewa kuingia sokoni mwezi huu na inategemea kuanza kuuzwa kwa dollar za marekani $129.99 sawa na TZS 299,000 bila kodi kwa external yenye GB 500, na dollar $299.99 sawa na TZS 670,000 bila kodi kwa external yenye TB 1, na dollar $399.99 sawa na takribani TZS 920,000 bila kodi kwa external yenye TB 2.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use