Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A90 5G

Zifahamu hizi hapa sifa pamoja na bei ya Samsung Galaxy A90 5G
Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A90 5G Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A90 5G

Kampuni ya Samsung tayari inazo simu 4 zenye uwezo wa mtandao wa 5G, Hivi karibuni kampuni hiyo imeongeza simu ya 5 na sasa kampuni hiyo inazo simu za Galaxy S10 5G, Galaxy Note 10 5G, Galaxy Note 10+ 5G na sasa Galaxy A90 5G.

Ingawa mtandao wa 5G kwa hapa Afrika na Tanzania kwa ujumla bado haujafika, lakini hebu tungalie sifa pamoja na bei za simu hii bora ya daraja la kati (mid-range smartphone) kutoka Samsung.

Kwa kuanza ngoja tuanze na kioo, Galaxy A90 5G inakuja na kioo cha Inch 6.7 ambacho kime-tengenezwa kwa teknolojia ya Super AMOLED ambacho pia kinakuja na resolution hadi ya pixels 1080 x 2400. Mbali na hayo Galaxy A90 5G inakuja na sensor ya fingerprint ambayo inapatikana chini ya kioo hicho ambacho kwa juu kinakuja na ukingo wa juu ambao unatumika kuhifadhi kamera ya selfie ya Megapixel 32 yenye uwezo wa kuchukua video za hadi 1080p@30fps.

Advertisement

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A90 5G

Kwa nyuma A90 5G inakuja na kamera tatu kamera kuu ikiwa inakuja na uwezo wa Megapixel 48, kamera ya pili ikiwa na uwezo wa Megapixel 8 na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 5. Kamera zote hizo zinasaidiwa na Flash ya LED flash pamoja na teknolojia za Panorama pamoja na HDR. Vilevile kamera zote kwa pamoja zinakuja na uwezo wa kuchukua video za hadi 4K ambayo ni sawa na kusema simu hii inakuja na uwezo wa kuchukua video za 2160p@30fps, 1080p@30/60fps (gyro-EIS) pamoja na 720p@960fps.

Kwa upande wa processor Samsung Galaxy A90 5G inaendeshwa na processor ya Qualcomm Snapdragon 855, processor ambayo inasaidiwa na RAM kati ya GB 6 au GB 8 pamoja na ukubwa wa ROM wa hadi GB 128. Ukubwa huo unaweza kuongezwa kwa kutumia memory card hadi ya GB 512 kwa simu yenye RAM ya GB 6 pekee, simu yenye RAM ya GB 8 yenyewe inakuja ikiwa haina sehemu ya kuweka Memory Card. Mbali na hayo sifa nyingine za Galaxy A90 5G ni kama zifuatazo.

Kampuni ya Samsung Yazindua Simu Mpya ya Galaxy A90 5G

Sifa za Samsung Galaxy A90 5G

  • Ukubwa wa Kioo – Inch 6.7 chenye teknolojia ya Super AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2400 pixels.
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (1×2.84 GHz Kryo 485 & 3×2.42 GHz Kryo 485 & 4×1.78 GHz Kryo 485).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm).
  • Uwezo wa GPU – Adreno 640.
  • Ukubwa wa Ndani – GB 128
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu mbili simu moja inakuja na RAM ya GB 6 na nyingine inakuja na RAM ya GB 8.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Megapixel 32 yenye f/2.0, HDR pamoja na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera tatu kwa nyuma moja ikiwa na Megapixel 48 yenye f/2.0, 26mm (wide), 1/2″, 0.8µm, PDAF na nyingine ikiwa na Megapixel 8 ambayo ni ultrawide, pamoja na Megapixel 5 ambayo ni depth sensor. Kamera zote zinasadiwa na Flash ya LED flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-po 4500 mAh battery yenye teknolojia ya Fast Charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE, aptX HD na GPS ya A-GPS, GLONASS, BDS. USB ya 2.0 Type-C 1.0 reversible connector.
  • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Black na White
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by),  Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Fingerprint, accelerometer, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G, 4G na 5G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Chini ya Kioo).

Bei ya Samsung Galaxy A90 5G

Kwa upande wa bei hadi sasa bado kampuni ya Samsung haijatangaza rasmi bei ya simu hii ingawa kwa mujibu wa tovuti ya Samsung simu hii inatarajiwa kuzinduliwa rasmu huko nchini korea ya kusini ambapo tayari teknolojia ya 5G inaendelea kufanyakazi. Kupata habari zaidi kuhusu bei ya simu hii endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujulisha pindi tutakapo pata bei halisi ya simu hii.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use