Kampuni ya Nokia Yazindua Simu Mpya za Nokia 220 4G na Nokia 105

Matoleo mpya ya simu za “Nokia ya Tochi”
Kampuni ya Nokia Yazindua Simu Mpya za Nokia 220 4G na Nokia 105 Kampuni ya Nokia Yazindua Simu Mpya za Nokia 220 4G na Nokia 105

Kama wewe ni mpenzi wa simu za Nokia basi ni muhimu kujua kuwa kampuni ya Nokia imeingiza sokoni simu mpya za Nokia 220 4G na Nokia 105. Simu hizi ni matoleo mapya ya simu za vitochi, simu ambazo zilitumiwa sana kwenye miaka ya nyuma.

Tokea kampuni ya Nokia ilipozindua simu mpya ya Nokia 3310, sasa imekuja na matoleo haya mapya ambapo Nokia 220 inakuja na uwezo wa mtandao wa 4G.

Advertisement

Mbali ya uwezo wa Mtandao Nokia 220 4G inakuja na Radio pamoja na tochi, huku battery yake ya 1200 mAh ikikuruhusu kutembelea kutumia 4G pamoja na kucheza game ya nyoka kwa muda mrefu. Sifa za Nokia 220 4G ni kama zifuatazo.

Sifa za Nokia 220 4G

  • CPU: One-core
  • RAM: 16 MB
  • Storage: 24 MB
  • Display: QQVGA, 2.4 inches
  • Camera: Rear VGA
  • OS: Feature OS
  • Radio: Yes FM Radio
  • Battery: Removable 1200 mAh

Kwa upande wa bei bado simu hii haijajulikana itauzwa kwa bei gani, ila unaweza kutegemea kuipata simu hii kuanzia shilingi za kitanzania Tsh 130,000 au zaidi.

Kwa upande wa Nokia 105 yenyewe ni simu ya kawaida sana, inakuja na mtandao wa 2G na ni simu bora sana kwa wasafiri au watu wanaotaka simu zinazodumu na chaji. Simu hii inakuja na battery ya 800 mAh, battery ambayo itakuwa inatumika tu kupiga simu, kusikiliza radio pamoja na kutumia tochi. Kama unataka simu hii basi hizi hapa ndio sifa za Nokia 105.

Sifa za Nokia 105

  • CPU: One-core
  • RAM: 4 MB
  • Storage: 4 MB
  • Display: QQVGA, 1.77 inches
  • Camera: No
  • OS: Nokia Series 30+
  • Radio: Yes FM Radio
  • Battery: Removable 800 mAh

Kwa upande wa bei simu hii bado bei yake haijatangazwa ila unaweza kuipata kwa bei ya makadirio kuanzia Shilingi za Tanzania Tsh 80,000 pamoja na kodi. Kumbuka simu hizi bado hazijafika kwa hapa Tanzania ila zitakapofika tegemea kupata habari kupitia hapa hapa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use