in

Jinsi ya Kujua Apps Zinazotumia Data kwa Wingi (Android na iOS)

Fahamu app hizo ili kuweza kuzuia data au bando kuisha kwa haraka

Jinsi ya Kujua Apps Zinazotumia Data kwa Wingi (Android na iOS)

Hapa Tanzania Tech tumeshaongelea sana tatizo la watu kulalamika kuhusu vifurushi vya bando au salio kuisha haraka bila hata kutumika kwa muda uliopangwa, vilevile katika kutafuta sababu tumeshaelezea sababu nyingi sana ikiwemo ile ya Data Roaming ambayo pengine hii ilionekana kuwa sababu kubwa kuliko zote inayo sababisha bando au salio kuisha kwa haraka.

Kwa leo hebu tuangazie upande mwingine ambao pia unaweza ukawa ni sababu kubwa ya data au bando lako pamoja na salio kuisha kwa haraka, upande huu sio mwingine ni Apps ambazo unatumia kwenye simu yako ya mfumo wa Android pamoja na iOS. Ukweli ni kwamba apps zinaweza kuwa ndio sababu ya bando lako kuisha kwa haraka hivyo ni vyema kujua app ipi inatumia bando kiasi gani ili kuweza kujua bando lako au salio linapokwenda zaidi.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha njia ambazo unaweza kutumia kuweza kujua ni app gani ambazo zinatumia data kwa wingi ili kusudi ujue ni hatua gani ya kuchukua. Kumbuka njia hizi zipo za Android pamoja na iOS hivyo fuatisha ile ambayo inaendana na kifaa unachotumia.

Kujua Apps Zinazotumia Data kwa Wingi (Android)

Mfumo wa Android unakuja na sehemu nyingi sana ambazo ukweli ni kwamba sio sehemu zote zinazojulikana na kila mtu. Kupitia simu yako ya Android unaweza kuona ni app gani inayotumia data kwa wingi bila hata ku-install programu yoyote kwenye simu yako.

Kwa kuanza ili kupata sehemu hii unatakiwa kuingia kwenye sehemu ya Settings kwenye simu yako ya Android. Kisha ingia kwenye sehemu ya Connections

Jinsi ya Kujua Apps Zinazotumia Data kwa Wingi (Android na iOS)

Kisha bofya sehemu ya Data Usage.

Jinsi ya Kujua Apps Zinazotumia Data kwa Wingi (Android na iOS)

Baada ya hapo tafuta sehemu iliyo andikwa Mobile data usage kisha bofya hapo.

Jinsi ya Kujua Apps Zinazotumia Data kwa Wingi (Android na iOS)

Baada ya hapo utaona ukurasa mpya ukiwa unachati maalum kuonyesha matumizi ya data au bando kwa muda maalum, chati hiyo ndio inayo onyesha matumizi ya data kwenye apps mbalimbali kupitia simu yako ya Android. Unachotakiwa kuangalia ni jina la kwanza la app iliyopo chini ya chati hiyo na ndio itakuwa app inayotumia kutumia data au bando kwa wingi zaidi.

Jinsi ya Kujua Apps Zinazotumia Data kwa Wingi (Android na iOS)

Kama unavyoweza kuona hapo juu kwenye simu hii, Mobile Hotspot and Tethering ndio inaonekana kutumia data kwa wingi kwa muda ambao picha hii ilichukuliwa, app ya Secure Folder liyokuwa juu yake kwa muda huo ilikuwa iki-update ndio maana unaweza kuiona juu ya app inayotumia data zaidi. Ni vizuri kuangalia apps tano za kwanza ili kuona app inayotumia data zaidi.

Kujua Apps Zinazotumia Data kwa Wingi (iOS)

Kwa upande wa iOS napo pia unatakiwa kuingia kwenye ukurasa wa Settings, kisha baada ya hapo bofya sehemu ya Cellular, alafu bofya sehemu ya Cellular Data. Baada ya hapo sehemu hiyo itaweza kuonyesha app inayotumia data kwa wingi zaidi. Ukibofya hapo pia utaweza kuona taarifa za apps husika na data inayotumia.

Kwa kufuata hatua hizi natumaini utaweza kuona apps mbalimbali za Android na iOS ambazo zitakuwa zinatumia data kwa wingi kwenye simu yako. Kumbuka kama hii haitoweza kuondoa tatizo la bando kuisha kwa haraka kwenye seimu yako unaweza kusoma kuhusu sehemu ya data roaming ambayo pia inapatikana kwenye simu zote za Android na iOS.

Jinsi ya Kujua Apps Zinazotumia Data kwa Wingi (Android na iOS)
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Maujanja ya WhatsApp Hambayo Ulikuwa Hujui (2023)

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment