in

Kutana na Kivinjari (Browser) Maalum kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu

Kivinjari hichi kitazuia kutembelea tovuti ambazo hazifuati maadili ya kiislamu

Kutana na Kivinjari (Browser) Maalum kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu

Kama wewe ni mmoja wa Waumini wa Dini ya Kiislamu basi ni muhimu kusoma makala hii, lakini hata kama wewe sio muislamu basi ni vizuri pia kusoma makala hii kwani nakuahidi utaweza kwenda kujifunza kitu hasa namna ya kutumia teknolojia kwa njia sahihi.

Sasa kama ulikuwa hujui, kuna aina mpya ya browser ambayo imetengenezwa maalum kwa waumini wa dini ya kiislamu. Browser hiyo au kivinjari hicho kinakupa uwezo wewe muslamu kufanya mambo mbalimbali ambayo pengine ulikuwa huwezi kufanya kwenye browser ya kawaida.

Browser hiyo inakuja na sehemu maalum za kuonyesha muda wa kuswali, pia utaweza kupata taarifa mbalimbali za habari za dini ya kiislamu, pamoja na kujifunza maneno mbalimbali kutoka kwenye kitabu kitakatifu cha Quran.

Kutana na Kivinjari (Browser) Maalum kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu

Mbali na hayo yote browser hiyo inayoitwa SalamWeb, itakupa uwezo wa kuwa salama mtandao kwa kuzuia kutenda dhambi kwa kutembelea tovuti ambazo hazi ruhusiwi kwa mujibu wa sheria za dini ya Kiislamu. Endapo mtu atafungua tovuti yenye mambo ambayo yanakatazwa, kivinjari hicho kitakupa ujumbe kwamba kutembelea tovuti hiyo ni kinyume na sheria za dini ya Kiislamu.

Video: Je Wajua Aina za Roboti Wanaofanana na Wanyama.?

Mbali na hayo SalamWeb inakuja na sehemu ya kuchat ambayo inawawezesha waislamu wote kwa pamoja kuchat kwa pamoja kupitia kivinjari hicho. Uzuri wa sehemu hii ni kuwa inaweza kuku unganisha na waislamu pekee waliopo karibu, takribani kilometa 1 toka ulipo.

Kutana na Kivinjari (Browser) Maalum kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu

Kivinjari hichi ni kuzuri sana kwa waislamu wote na inakupa muonekano mzuri na bora kama ilivyo Google Chrome, kama wewe ni baba au mama mwenye mtoto ni vyema kutumia kivinjari hichi kwani kitasaidia mtoto kukuwa kwa kufuata maadili ya dini ya Kiislamu. Kama unataka kudownload app hii inapatikana kwenye mifumo yote ya Android, iOS, macOS pamoja na Windows.

SalamWeb – Android

SalamWeb – iOS

SalamWeb – Windows / Mac

Download Programu ya Salamweb Mac au Windows hapa

Na hiyo ndio browser au kivinjari cha Salamweb ambacho ni maalum kwa waumini wa dini ya kiislamu. Kama umefanikiwa ku-install kivinjari hicho tuambie kwenye maoni hapo chini unaonaje kivinjari hichi. Kama unataka kujua makala zaidi za je wajua basi soma hapa.

Jackline John

Written by Jackline John

Jack ni mpenzi wa teknolojia napenda kuandika kuhusu maujanja, simu na kompyuta. Unaweza kunipa maujanja kupitia [email protected]

Toa Maoni Hapa

Avatar

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.