in

WhatsApp Kuacha Kufanyakazi Kwenye Windows Phone Zote

Pia zipo simu nyingine za Android pamoja na iOS ambazo hazitopokea WhatsApp

WhatsApp Kuacha Kufanyakazi Kwenye Windows Phone Zote

WhatsApp imekuwa ikifanya mabadiliko kila toleo jipya la Android linapotoka, mabadiliko mapya kipindi hichi yanalenga kwa watumiaji wa simu za Windows Phone.

Kwa mujibu wa ripoti kupitia blog ya WhatsApp, Watumiaji wa simu hizo za zamani hawatoweza kutumia programu ya WhatsApp kwenye simu zao hapo ifikapo tarehe 31 December  2019. Mbali na Windows Phone pia WhatsApp imeongeza baadhi ya simu za Android na iOS ambazo nazo pia zitasimama kutumia programu ya WhatsApp ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2020.

Simu hizo ni pamoja na simu zote zenye kutumia mfumo wa Android kuanzia toleo la 2.3.7 na kushuka chini, pia zipo simu za iPhone ambazo zinatumia mfumo wa iOS kuanzia iOS 7 na kushuka chini. Pia WhatsApp imeongeza kuwa kwa kuwa imeacha kutengeneza programu ya WhatsApp kwa ajili ya simu hizo, basi inawezekana programu hiyo ikasimama kufanyakazi kwenye simu hizo mapema hata kabla ya kipindi kilicho tajwa kufikia.

Kwa sasa ni vizuri kama kubadilisha simu kama unatumia moja ya simu yenye mfumo uliyo tajwa hapo juu. Unaweza kusoma hapa kujua simu za bei rahisi za Android ambazo unaweza kuendelea kutumia programu yako ya WhatsApp.

Apps Muhimu kwaajili ya Mwezi wa Ramadhani (2023)

Written by Jackline John

Jack ni mpenzi wa teknolojia napenda kuandika kuhusu maujanja, simu na kompyuta. Unaweza kunipa maujanja kupitia [email protected]

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.