Japan Kuanza Kutumia Namba za Simu Zenye Tarakimu Zaidi ya 11

Inasemekana Japan imeanza kuishiwa na namba zenye tarakimu 11
Japan Kuanza Kutumia Namba za Simu Zenye Tarakimu Zaidi ya 11 Japan Kuanza Kutumia Namba za Simu Zenye Tarakimu Zaidi ya 11
Picha @WikiHow

Namba za simu huwa na kawaida ya kuwa na tarakimu 10 au zaidi pale zinapokuwa na namba za utambulisho wa nchi. Lakini hivi karibuni nchini Japan mambo yameanza kufikiriwa tofauti kwani nchini miaka ya karibuni wananchi wa nchini humo wataanza kutumia namba za simu zenye tarakimu zaidi ya 11.

Kwa mujibu wa tovuti ya Japan Times, inasemekana kwa sasa nchini humo namba za simu zina tarakimu 11 huku wazo la kuwa na namba yenye tarakimu 14 yakiwa tayari wamesha anza kufanyiwa kazi. Namba ya tarakimu 14 hanusisha na namba za utambulisho wa nchi ambazo huwa kabla ya namba ya simu ya mtu.

Kwa mujibu wa tovuti hiyo, inasemekana hatua hii imekuja baada ya mamlaka ya mawasiliano nchini humo kuona kuwa namba hizo zenye tarakimu 11 zinawezekana kuisha kati ya kipindi cha mwaka 2021 na mwaka 2022.

Advertisement

Hata hivyo tayari kampuni kubwa za simu nchini humo kama vile NTT Docomo, KDDI na SoftBank zimesha kubaliana na mpango huo wa kutengeneza namba zaidi ya bilioni 10 zenye tarakimu 14, huku namba hizo zikisemekana kuanzia na namba “020.”

Kwa sasa hapa kwetu Tanzania bado tunatumia namba zenye tarakimu 10, huku ikiwa inaonekana bado namba hizo hazija tarajiwa kuisha kwani hakuna taarifa yoyote yenye kueleza hatua kama hii.

Hata hivyo ni jambo la kufikiria, hivi itakuwaje pale mtu hapa Tanzania atakapokuwa na namba yenye tarakimu 14 yani mfano 07001234567890, kama unavyoweza kuona hii itakuwa ngumu sana kwa wengi wetu kukariri namba hii na wakati mwingine itakuwa kama una hesabu namba wakati unamtajia mtu namba yako.

Anyway..najua unajua sasa. Kama unataka kujua mambo mengine ambayo ulikuwa huyajui kuhusu teknolojia unaweza kutembelea ukurasa wetu wa Instagram hapa na utaweza kujionea mambo mbalimbali ya teknolojia ambayo ulikuwa huyajui.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use