Lenovo Yazindua Simu Mpya ya Lenovo Z6 Pro Yenye Kamera Nne

Zifahamu hizi hapa sifa pamoja na bei ya Lenovo Z6 Pro
Lenovo Yazindua Simu Mpya ya Lenovo Z6 Pro Yenye Kamera Nne Lenovo Yazindua Simu Mpya ya Lenovo Z6 Pro Yenye Kamera Nne

Niwazi kuwa mwaka 2019 ni mwaka wa simu janja nyingi kuwa na kamera zaidi ya mbili na inaonekana kama mtindo wa simu kuwa na kamera moja sasa ni mtindo wa kizamani kwani, hadi sasa asilimia 90 ya simu zote zilizotoka zinakuja na kamera mbili au zaidi.

Kwa kampuni ya Lenovo mambo hayajabadilika sana kwani kampuni hiyo nayo imekuja na simu mpya ya Lenovo Z6 Pro ambayo inakuja na kamera nne za kisasa na zenye uwezo mkubwa sana. Tukianza na kamera ya mbele, simu hii inakuja kamera yenye uwezo wa Megapixel 32 yenye uwezo wa kuchukua video za 1080p@30 huku ikiwa na teknolojia ya HDR.

Kwa nyuma Lenovo Z6 Pro inakuja na kamera nne ambapo kamera ya kwanza inakuja na uwezo wa Megapixel 48, ya pili inakuja na Megapixel 16 huku nyingine mbili zikiwa na Megapixel 8 na Megapixel 2. Pia simu hii inakuja na TOF camera sensor ambayo hii ni kwa ajili ya kusaidia kupiga picha kwenye mwanga hafifu.

Advertisement

Lenovo Yazindua Simu Mpya ya Lenovo Z6 Pro Yenye Kamera Nne

Mbali na kamera Lenovo Z6 Pro inakuja na processor ya Snapdragon 855 chipset, ambayo inasaidiwa na RAM ya kuchagua kati ya GB 12, GB 8 au GB 6, vilevile simu hii inakuja na ukubwa wa ROM wa kuchagua kati ya GB 512 na GB 128. Ukubwa huu unaweza kuongezewa kwa memory card ya MicroSD Card yenye ukubwa wa hadi GB 512. Mbali na hayo sifa nyingine za simu hii ni kama zifuatazo.

Lenovo Yazindua Simu Mpya ya Lenovo Z6 Pro Yenye Kamera Nne

Sifa za Lenovo Z6 Pro

  • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.39 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~403 ppi density).
  • Mfumo wa Uendeshaji – Android 9.0 (Pie)
  • Uwezo wa Processor – Octa-core (1×2.84 GHz Kryo 485 & 3×2.42 GHz Kryo 485 & 4×1.8 GHz Kryo 485).
  • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM855 Snapdragon 855 (7 nm) Chipset.
  • Uwezo wa GPU – Adreno 640.
  • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na ukubwa wa ndani wa GB 128 na nyingine ikiwa na ukubwa wa ndani wa GB 512 zikiwa zina uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 512.
  • Ukubwa wa RAM – Ziko simu za aina mbili, simu moja inakuja na RAM ya GB 12 na nyingine inakuja na RAM ya GB 8 ua GB 6.
  • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ipo kamera moja ya Megapixel 32 yenye f/2.0 huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za 1080p@30fps.
  • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera nne kamera moja inakuja na Megapixel 48 yenye uwezo f/1.8, PDAF na nyingine inakuja na uwezo wa Megapixel 16 yenye f/2.2, 12mm (ultrawide), nyingne inakuja na Megapixel 8 ambayo ina f/2.4, (telephoto), PDAF na kamera ya mwisho ikiwa na Megapixel 2 ambayo ni f/1.8, 2.9µm, OIS, PDAF (dedicated video camera) huku kamera zote zikiwa na uwezo wa kuchukua video za 4K na 1080p@30fps. Flash ya Dual-LED dual-tone flash.
  • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 4000 mAh battery yenye uwezo wa Fast battery charging.
  • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS. 2.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
  • Rangi – Inakuja kwa mbili za Red na Green
  • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by)
    ,Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
  • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Infrared face recognition, fingerprint (under display), accelerometer, gyro, proximity, compass.
  • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
  • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Mbele Kwenye Kioo).

Bei ya Lenovo Z6 Pro

Kwa mujibu wa Lenovo, Lenovo Z6 Pro ni Tofauti na Lenovo Z5 Pro kwani simu hii inategemewa kupatikana kwanza nchini China na itakuwa inapatikana kwa bei ya kuanzia Yuan CNY2,899 ambayo ni sawa na Tsh 994,000 bila kodi kwa toleo la simu hii lenye RAM ya GB 6 na ukubwa wa ROM wa GB 128. Toleo la RAM ya GB 8 na ukubwa wa ROM wa GB 128 itauzwa kwa Yuan CNY2,999 ambayo ni sawa na Tsh 1,028,000 bila kodi.

Toleo la mwisho lenye RAM ya GB 12 na ROM ya GB 512 litauzwa kwa Yuan CNY4,799 ambayo ni sawa na Tsh 1,645,000 bila kodi. Kumbuka bei hizi zinaweza kubadilika kwa hapa Tanzania.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use