in

Lenovo Z5 Pro Simu Mpya Kutoka Kampuni ya Lenovo

Simu nyingine yenye kamera zinazojificha…

Lenovo-Z5-Pro sifa na bei

Kampuni ya Lenovo kwa mara nyingine tena hivi leo imezindua simu yake mpya ya Lenovo Z5 Pro simu inayokuja na mfumo wa kamera kama wa simu ya Oppo Find X. Simu hii mpya ya Lenovo Z5 Pro inakuja na kioo kikubwa cha inch 6.39 ambacho kimetengenezwa kwa teknolojia FHD chenye resolution ya 1080 x 2340 pixel.

Simu hii ya Lenovo Z5 Pro inaendeshwa na processor ya Snapdragon 710 ambayo inasaidiwa na RAM ya GB 6 pamoja na ukubwa wa ndani wa GB 128 ukubwa ambao hauongezwi na memory card.

Kwa nyuma simu hii ya Lenovo Z5 Pro inakuja na kamera mbili, kamera moja inakuja na Megapixel 16 na nyingine inakuja na Megapixel 24 huku kwa mbele simu hii ikiwa na kamera mbili pia huku kamera moja ikiwa na Megapixel 16 na nyingine ikiwa na Megapixel 8, huku zote zikiwa kwenye kava linaloficha kamera hizo hadi pale unapotaka kuzitumia.

Mbali na hayo simu hii pia inakuja na sehemu ya fingerprint kwenye kioo ambayo inaongezewa ulinzi na ulinzi wa kutambua uso. Zaidi ya hapo simu hii inaendeshwa na battery yenye uwezo wa 3,350 mAh battery ambayo inakuja na uwezo wa Fast battery charging.

Kwa upande mfumo wa uendeshaji simu hii ya Lenovo Z5 Pro inatumia mfumo wa Android Oreo mfumo ambao juu yake kuna mfumo wa lenovo wa ZUI 10, Sifa nyingine za simu hii ya Lenovo Z5 Pro ni kama zifuatazo.

Sifa za Lenovo Z5 Pro

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.39 chenye teknolojia ya AMOLED capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 1080 x 2340 pixels, na uwiano wa 19.5:9 ratio (~403 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android 8.1 (Oreo)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core (2×2.2 GHz 360 Gold & 6×1.7 GHz Kryo 360 Silver).
 • Aina ya Processor (Chipset) – Qualcomm SDM710 Snapdragon 710 (14 nm) Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 616.
 • Ukubwa wa Ndani – Ziko simu za aina mbili moja ikiwa na ukubwa wa ndani wa GB 64 na nyingine ikiwa na ukubwa wa ndani wa GB 128 ikiwa haina uwezo wa kuongezewa na memory card.
 • Ukubwa wa RAM – RAM ya GB 6.
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele – Ziko kamera mbili moja inakuja na Megapixel 16 yenye uwezo f/2.2 na nyingine inakuja na uwezo wa Megapixel 8 huku ikiwa na uwezo wa kuchukua video za [email protected]
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 16 MP, f/1.7, 1/2.8″, 1.12µm, PDAF na nyingine inakuja na Megapixel 25 yenye f1/2.8″, 0.9µm huku kamera zote zikiwa zinasaidiwa na Flash ya Dual-LED dual-tone flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Po 3350 mAh battery yenye uwezo wa Fast battery charging.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 5.0, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, GLONASS. 2.0, Type-C 1.0 reversible connector, USB On-The-Go.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi moja ya Black.
 • Mengineyo – Haina Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by)
  ,Haina sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Aina za Sensor – Inakuja na sensor za Infrared face recognition, fingerprint (under display), accelerometer, gyro, proximity, compass.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Inayo Fingerprint (Mbele Kwenye Kioo).
Usinunue Simu ya Android au iPhone ya Zamani

Bei ya Lenovo Z5 Pro

Kwa upande wa bei Lenovo Z5 Pro inakuja na ikiwa inauzwa Yuan ya China CNY 1,998 ambayo ni sawa na Tsh 661,000 bila kodi kwa toleo lenye ukubwa wa ndani wa GB 64, Kwa simu yenye ukubwa wa ndani wa GB 128 yenyewe itauzwa kwa Yuan ya China CNY 2,298 sawa na Tsh 761,000 bila kodi. Kumbuka bei inaweza kubadilika kwa Tanzania kutokana na viwango vya kubadilisha fedha pamoja na kodi.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.