Instagram Yaja na Aina Mpya ya Stika za Kuuliza Maswali ya Kuchagua

Sasa utaweza kuuliza maswali ya kuchagua kwenye ukurasa wako wa Instagram
Instagram Yaja na Aina Mpya ya Stika za Kuuliza Maswali ya Kuchagua Instagram Yaja na Aina Mpya ya Stika za Kuuliza Maswali ya Kuchagua

Mwaka 2017 Instagram ilianzisha stika za maswali au Poll Stickers ambazo zinamruhusu mtumiaji wa mtandao wa Instagram kuweza kuuliza maswali kupitia sehemu ya Stories, Lakini kama haitoshi hivi leo instagram imekuja na aina nyingine ya Stika za maswali ambazo zina kuwezesha kuuliza maswali ya kuchagua kupitia sehemu ya Stories.

Stika hizo mpya ambazo tayari zinapatikana kwenye mtandao wa Instagram, zina kuwezesha kuuliza maswali ya kuchagua huku ukiweka jibu la swali lako kwa ajili ya wafuasi wako kuweza kuona pale watakapo chagua jibu ambalo sio sahihi.

Instagram Yaja na Aina Mpya ya Stika za Kuuliza Maswali ya Kuchagua

Advertisement

Sehemu hiyo mpya ya kuuliza maswali ambayo imepewa jina la Quiz sticker kwa sasa tayari inapatikana kwa watumiaji wote na ili kuweza kuipata unahitajika kutengeneza Stories kwenye ukurasa wako wa instagram, kisha chagua sehemu ya Stika kisha utaona stika mpya iliyo andikwa QUIZ kwa herufi kubwa.

Chagua hapo kisha andika swali lako kisha andika majibu yako kisha weka alama ya tiki kwenye jibu la swali lako kisha unaweza kubadilisha rangi ya juu ya swali lako kwa kubofya kitufe cha rangi kilichopo juu katikati, baada ya kumaliza yote utamaliza kwa kubofya Done na moja kwa moja utakuwa umeweza kuuliza maswali ya kuchagua kupitia sehemu hii mpya ya Quiz sticker.

Sehemu hii haitaji ku-update app ya instagram, hivyo kama kwa namna yoyote bado hujaona sehemu hiyo basi usijali kwani itawezeshwa baada ya muda mfupi.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use