in

Oppo Yatangaza Kuja na Kampuni Mpya ya Simu ya ‘Reno’

Jiande kwa simu mpya kutoka kampuni mpya ya Oppo Reno

Oppo Yatangaza Kuja na Kampuni Mpya ya Simu ya 'Reno'

Kampuni ya kutengeneza simu ya Oppo, hivi leo imetangaza ujio wa kampuni mpya ya simu ambayo itakuwa ni sehemu ya kampuni ya Oppo. Kampuni hiyo inafahamika kwa jina la Reno ambapo simu yake ya kwanza inatarajiwa kutoka hivi karibuni.

Oppo Yatangaza Kuja na Kampuni Mpya ya Simu ya 'Reno'

Kwa sasa bado haijafahamika kuwa simu hiyo itaonekanaje na itakuwa inapatikana wapi, ila kwa mujibu wa tetesi mbalimbali, inasemekana kuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Oppo Brian Shen aliandika kwenye mtandao wa Weibo kuwa, Simu hiyo inatarajiwa kuja na sifa kama processor ya Snapdragon 855 pia simu hiyo itakuja na teknolojia mpya ya ku-zoom kwenye kamera zake teknolojia ambayo ilionyeshwa kwenye mkutano wa MWC (2019).

Mbali na hayo, inasemekana kuwa simu hiyo itakuja na battery yenye uwezo wa 4065mAh huku ikiwa na teknolojia za fast charging na nyingine kama hizo. Simu hiyo inasemekana kutoka rasmi mwezi wa nne na inategemea kuuzwa kwa zaidi ya nakala milioni 1.

[rafflepress id=”1″]

Kitendo cha kampuni ya Oppo kuwa na kampuni ya ziada kinashangaza kidogo kwani Hata kampuni ya Oppo ni sehemu ya kampuni ya BBK Electronics, kampuni ambayo inamiliki kampuni kama OnePlus, Vivo pamoja na OPPO Electronics Corp. Anyway itakubidi tusubiri mpaka hapo simu hii itakapo toka.

Fahamu eSIM Mfumo Mpya wa Laini za Simu za Kidigitali

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment