in

Picha Yenye Like Nyingi Instagram Ina Thamani ya Tsh Bilioni 23

Kwa sasa picha hiyo yenye like nyingi inakaribia like zaidi ya Milioni 52

picha ya yai yenye like nyingi instagram

Picha ya yai ambayo sasa ndio picha inayoongoza kwa kuwa na like nyingi kwenye mtandao wa Instagram, hivi karibuni inasemekana kufanya akaunti yenye picha hiyo kukadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya dollar za marekani milioni $10 ambayo ni sawa na zaidi ya Bilioni 23 za kitanzania.

Kwa mujibu wa tovuti ya papermag, kwa sasa kampuni nyingi za matangazo ya biashara zimekuwa zikitaka kufanya kazi na akaunti hiyo ambayo sasa inapost picha za yai likiwa linavunjika. Kwa mujibu wa tovuti hiyo kikubwa kinacho gombaniwa na makampuni hayo ya matangazo ni nafasi ya kuonekana ndani ya yai hilo pale picha ya yai hilo likiwa limepasuka kabisa itakapo wekwa.

Picha Yenye Like Nyingi Instagram Ina Thamani ya Tsh Bilioni 23

Kuonekana huko ndani ya yai hilo ndipo kunafanya thamani ya kuweza kuonekana kuwa zaidi ya dollar za marekani milioni $10. Kwa sasa zipo kampuni mbalimbali za marekani ambazo zinataka kuonyesha mambo mbalimbali ya upinzani wa kisiasa, huku makampuni mengine yakitaka kuonyesha bidhaa zao mbalimbali.

Njia Mpya ya Kutengeneza Pesa Kupitia YouTube Shorts Video

Mpaka sasa bado hakuna taarifa zaidi juu ya mmiliki au mwenye akaunti hiyo ya world_record_egg, ila kwa mujibu wa ripoti kutoka tovuti ya abc11, mwenye akaunti hiyo inasemekana kuwa inaishi kwenye mji wa London na alipata wazo la kuja na akaunti hiyo baada ya kusoma makala ya picha 20 zenye like nyingi kwenye mtandao wa Instagram.

Hadi sasa picha hiyo yenye like nyingi kuliko picha zote instagram, inayo likes zaidi ya milioni 51 huku ikikaribia sana kufikia milioni 52.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.