Sasa Unaweza Kujua Kama Password Zako Zimedukuliwa

Kama wewe ni mtumiaji wa programu ya Google Chrome unaweza kutumia njia hii
Google Password Checker Google Password Checker

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wamewahi kupata athari ya kudukuliwa au ku-hackiwa akaunti mbalimbali, sasa Google imeleta urahisi wa kuweza kujua kama password au nywila unazo tumia kwenye akaunti zako kama zimedukuliwa.

Hivi karibuni Google kupitia tovuti yake ilitoa taarifa kuhusu udukuaji mpya ambapo ulitokea ambao ulifanya watu wanaotumia kivinjari cha Google Chrome kubadilisha baadhi ya nywila au password wanazotumia kwenye akaunti mbalimbali mtandaoni. Kwa sababu ya udukuaji huo, Google ilikuja na njia mpya ambayo inaweza kuonyesha kama password unazo tumia kwenye akaunti zako mbalimbali kama ziko salama.

Kupitia kivinjari cha Google Chrome, Google imeleta aina mpya ya Extension ambayo itakuwa maalum kwa watumiaji wa kivinjari hicho, extension hiyo inayoitwa Password Checkup inauwezo wa kuangalia password kwenye akaunti zako mbalimbali na kukupa taarifa kama password zako haziko salama.

Advertisement

password checkup

Kama unavyojua kuhusu extension, Password Checker inapatikana kwa watumiaji wa kompyuta wa kivinjari cha chrome na unaweza kuweka kwenye kompyuta yako sasa ili kuweza kujua usalama wa akaunti zako mbalimbali. Unaweza kobofya link hapo chini kama unatumia kompyuta, kama unatumia simu extension hiyo haitaweza kufanya kazi.

Unknown app
Price: Free

Kwa mujibu wa tovuti ya Cnet, Google inatumia data kazi yenye password na username zilizo dukuliwa zaidi ya bilioni 4 ili kuweza kujua password ambazo tayari zimedukuliwa. Kwa mujibu wa tovuti hiyo, Google imetumia datakazi hiyo kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita kulinda watumiaji wa Google ambao wanaweza kuathirika na udukuaji wa aina yoyote.

password-checkerKwa sasa bado hakuna taarifa zaidi kuhusu njia hii kuja kwa watumiaji wa simu za mkononi, ila pengine siku za karibuni njia hii inaweza kuletwa kwa watumiaji wote. Kwa habari zaidi endelea kutembelea Tanzania Tech kila siku.

Maujanja : Jifunze Njia ya Kuangalia Kama Barua Pepe Yako Imedukuliwa

https://youtu.be/U4SgZ_VEzbM

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

Pata Habari za Teknolojia Kupita Barua Pepe

By pressing the Subscribe button, you confirm that you have read and are agreeing to our Privacy Policy and Terms of Use