in

Kutana na USB Flash Kubwa kuliko Zote Duniani Yenye TB 4

Kwa sasa hii ndio inashikilia chat ya flash kubwa kuliko zote duniani

Kutana na USB Flash Kubwa kuliko Zote Duniani Yenye TB 4

Ni wazi kuwa teknolojia inakuwa kila siku, Miaka ya karibuni tulisikia USB flash drive yenye TB 1 ndio flash kubwa zaidi, miezi michache baadae tukasikia Flash ya TB 2 ndio flash kubwa kuliko zote duniani. Lakini kama haitoshi sasa mwaka 2019 kuna USB flash nyingine ambayo sasa ndio kubwa zaidi duniani yenye ukubwa wa TB 4.

Kupitia mkutano wa CES 2019 kampuni ya Western Digital imezindua USB flash Drive ya SanDisk ambayo inakuja na uwezo wa TB 4 kuhu ikiwa ndio flash Drive iliyoshikilia taji la kuwa flash yenye ukubwa mkubwa zaidi Duniani.

Install Android App
Price: Free
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot
  • Nyimbo Mpya Screenshot

flash ya TB 4

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali inasemekana kuwa Flash Drive hiyo inakuja na speed kubwa na unaweza kuhifadhi vitu mbalimbali bila kuwa na wasiwasi wa speed yake wakati wa ku-copy. Lakini pamoja na yote hayo bado mpaka sasa haijatangazwa kama flash hii itaingia sokoni ila kwa mujibu wa Techradar, uwezekano wa flash hii kuingia sokoni ni mdogo sana kutokana na bei yake kukadiriwa kuwa kubwa sana.

Flash ya TB 4 kubwa zaidi duniani Pic 1

Kwa sasa kama unataka kununua flash kutoka Western Digital yenye ukubwa wa TB 1 unaweza kuipata kwa dollar za marekani $400 ambayo ni sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 920,000, sasa hadi hapo unaweza kuona bei ya TB 4 lazima itakuwa ni kubwa zaidi.

Kujua haya na mengine mengi hakikisha unaendelea kutembelea Tanzania Tech, pia unaweza kusoma ukurasa wetu wa CES 2019 ili kujua yote yanayoendelea kwenye mkutano wa CES unaofanyika huko Las Vegas nchini Marekani.

Kutana na USB Flash Kubwa kuliko Zote Duniani Yenye TB 4
Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Elon Musk Azindua Mfumo wa Akili Bandia (AI) xAI Grok

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.