in

Jinsi ya Kutumia Kamera ya Simu Kama WebCam ya Kompyuta

Kompyuta yako haina WebCam..? Usijali fuata hatua hizi kuweka webcam

simu ya android kama webcam

Ni kweli kwamba kuna wakati unahitaji kamera ya kompyuta hii inaweza ikiwa ni kwaajili ya kazi au kwaajili ya mambo mengine ya muhimu. Kwa sababu hii unaweza ukawa na kompyuta lakini haina sehemu ya kamera hivyo makala hii itaweza kukusaidia kubadilisha kamera ya simu yako kuwa kamera ya kompyuta yako maarufu kama WebCam. Basi bila kupoteza muda twende tuka jifunze hatua kwa hatua.

Hatua ya kwanza unahitaji kudownload programu ya DroidCam programu hii inapatikana kwa kulipia na pia inapatikana bure, unaweza kuchagua toleo unalotaka kulingana na uwezo wako. Unaweza kupakua programu ya bure kupitia link hapo chini.

  • DroidCam Wireless Webcam

Baada ya kudownload app hiyo ya DroidCam kwenye simu yako ya Android sasa endelea kwenye hatua inayofuata. Kwenye hatua inayofuata pakua programu nyingine kwaajili ya kompyuta yako, unaweza kupata link ya programu hiyo HAPA. Baada ya kupakua programu hiyo na kuinstall kwenye kompyuta yako sasa endelea kwenye hatua inayofuata.

Download Apps Play Store Ambazo Hazipatikani Tanzania

Baada ya kuinstalll programu ya DroidCam kwenye kompyuta yako ifungue na utaletewa sehemu yenye kutaka uweke Device IP, ili kupata hiyo Device IP fungua App ya DroidCam kwenye simu yako kisha weka WiFi IP zinazo onekana kwenye app hiyo, andika namba hizo kwa usahihi pamoja na nukta zake kwenye kompyuta na moja kwa moja weka tiki sehemu ya Audio kama unataka kuweka na sauti kisha bofya Start kwenye programu hiyo kwenye kompyuta yako.

Baada ya hapo utaweza kuona picha ya kwenye simu yako kupitia kompyuta yako, unaweza kubadilisha mpangilio kwa kuchangua kuunganisha simu yako kwa waya au kwa kutumia WiFi. Kwa kutumia waya bofya sehemu ya pili juu kushoto na utatakiwa kutumia waya wa simu yako kuweza kuona picha kwenye kompyuta yako.

Mpaka hapo utakuwa umeweza kuweka webcam kwenye kompyuta yako kwa kutumia simu yako ya mkononi. Kumbuka programu hii hatumii internet hivyo unaweza kuitumia kwa muda wowote ule. That’s it guys kama maujanja haya yamekusaidia tuambie kwenye maoni hapo chini pia tembelea Tanzania Tech kila siku kwa maujanja zaidi.

Amani Joseph

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Avatar

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.