in

Soma Habari Zote Hapa Tanzania Kupitia Gazeti App

Sikiliza Radio, Soma Blogs, Angalia TV pamoja na Video Mbalimbali

App Mpya ya Gazeti App

Kupata habari imekuwa ni rahisi sana siku hizi, hii inatokana na kuwepo kwa vyanzo vingi vya habari kiasi kwamba ni lazima utaweza kupata habari kupitia vyanzo hivyo. Lakini wote tunajua ni ngumu sana kupata habari kwa ukamilifu kwa kuwa haiwezekani kutembelea tovuti zote hizo kwa pamoja ndio maana tunakuletea App ya Gazeti.

Gazeti ni App itakayokupa uwezo wa kusoma habari mbalimbali kwa urahisi kutoka tovuti mbalimbali za hapa nchini Tanzania, Mbali na tovuti app ya Gazeti inakupa uwezo wa kuangalia TV, Video pamoja na kusikiliza Radio Mbalimbali za hapa nchini Tanzania.

Kifupi ni kwamba App ya Gazeti inayo kila kitu ambacho unaweza ukawa unahitaji ili kuweza kupata habari mbalimbali za hapa nchini Tanzania, Sasa huna haja ya kuwa na app nyingi kwenye simu yako bali sasa unaweza kuwa na App moja yenye kukupa habari mbalimbali kwa urahisi zaidi.

Kwa sasa App ya Gazeti Inapatikana Kupitia Play Store na unaweza kuipata moja kwa moja kwa kubofya link Hapo chini. Kwa watumiaji wa iOS App hii inatarajiwa kuwafikia siku za karibuni.

  • Gazeti – Android
Kivinjari (Browser) Maalum kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.