in

Mabadiliko Mapya Kwenye Toleo Jipya la App ya Tanzania Tech

Update sasa app ya Tanzania Tech ili kupata muonekano mpya

App mpya ya tanzania tech

Habari njema kwa watumiaji na wapenzi wa tovuti ya Tanzania Tech sasa tunakuletea toleo jipya la App ya Tanzania Tech. Toleo hili jipya ambalo lina namba za toleo Version 1.50B1 linakuja na maboresho mapya pamoja na muonekano mpya kabisa.

Lakini kabla ya kujua kuhusu mabadiliko ya App yetu ya Android ni vyema tukashiriki nanyi kuhusu mafanikio yetu ya hivi karibuni. Kupitia soko la Play Store Tanzania Tech tumefanikiwa kufikia Downloads 5000 na kwa sababu hii na nyingine nyingi tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kwa wasomaji wetu kwani mmetupa moyo sana na ukweli mungu awabariki sana.

Mmekuwa pamoja nasi kuanzia tumeanza hadi sasa na hii inaonyesha kuwa mnathamini cha nyumbani na tuna ahidi kuwa tutaendelea kutunza thamani yenu kwetu na tutaendelea kuwaletea mambo mazuri kila siku.. Tunashukuru sana na tutaendelea kufanya mamboresho ya App yetu kulingana na maoni mtakayo endelea kutupa kupitia Play Store.

Basi baada ya kusema hayo sasa twende tukaangalie App Mpya ya Tanzania Tech, App hii ya sasa imetengenezwa kwa ustadi mkubwa ili kukithi haja za wasomaji wetu ikiwa pamoja na kutoa urahisi wa kutumia app hii. Muonekano wa sasa pia umabadilika kidogo lakini hakuna chochote kilicho ondolewa zaidi ya kuboreshwa zaidi.

  • Muonekano Mpya

Muonekano wa Toleo Jipya la App ya Tanzania Tech umeboreshwa zaidi na sasa unaweza kutumia app hii kwa urahisi kwa kutumia Menu mpya ambayo inapatikana kwa chini kabisa ya kioo cha simu yako. Menu hii inatumiaka kuendesha kila kitu kwenye app hii uku ukiwa na ukurasa mpya wa Mpangilio ambapo hapo ndio patakuwa na kila kitu kama vile akaunti za mitandao ya kijamii za Tanzania Tech, Maktaba kwaajili ya kusoma habari bila internet, Soma usiku au Night Mode ambayo hii itabadilisha app ya Tanzania Tech kuwa rahisi kutumia hasa wakati wa usiku.

Mbadala wa (IDM) Download Kwa Haraka Kwenye Kompyuta

Mbali na hayo App hii mpya inakuja na menu mpya kwenye sehemu hiyo ya Mpangilio, kupitia sehemu hiyo utaona sehemu ya Taarifa Mpya hii inakupa uwezo wa kuzima na kuwasha taarifa mpya au Notification kwenye App yako. Vilevile utaweza kuona sehemu mpya ya Forums ambayo hii itakupa uwezo wa kwenda kwenye app ya Forums ya Tanzania Tech kwaajili ya kuuliza maswali mbalimbali. Mbali na hayo kwa juu utaona sehemu ya kuingia na kutoka kwenye app ya Tanzania Tech huku ikiwepo na sehemu yenye picha yako kama umeingia kwa kutumia mitandao ya kijamii.

  • Mabadiliko Mengine

Mbali na hayo, yapo mabadiliko mengine madogo madogo ambayo yapo kwenye toleo hili jipya, mabadiliko hayo ni kama jinsi makala zinavyofunguka kuna utofauti kidogo. Pia sasa utaweza kupata taarifa zote kwenye sehemu moja, yaani pale utakapo pokea notification na ikatokea ujaisoma unaweza kuipata kwenye sehemu ya taarifa ndani ya app hii mpya.

  • Matatizo Yanayojulikana

Kila mabadiliko yanakuja na matatizo lakini kwa upande wa App hii mpya haina matatizo makubwa mpaka sasa. Baadhi ya matatizo ni pale unapo update.. mara baada ya ku-update kutoka toleo la zamani fungua app hiyo kisha ikifika kwenye logo ya Tanzania Tech na ukaona imekaa kwa muda funga na fungua tena app hiyo na kutakuwa hakuna tatizo tena kama hilo.

Apps Nzuri za Android Kwaajili ya Kulinda Afya Yako

Pia wakati mwingine kama unaona makala haisomi kwa muda au haisomi kwa wakati unaweza kufanya hatua hiyo hiyo ya kufunga na kufungua kwa upya. Kwa sasa tuna andaa toleo lingine jipya ambalo litakuwa linakuja na maboresho zaidi ikiwa pamoja na kutatua tatizo hili, Kwa sasa kama unataka kupakua toleo jipya la App ya Tanzania tech unaweza kubofya hapo chini na utapalekwa kwenye ukurasa wa Play store kisha bofya sehemu ya Update..

  • Tanzania Tech – Android

Vilevile kama unataka kujiunga na toleo la majaribio la Tanzania tech unaweza kujiunga kwa kubofya LINK HAPA, Kumbuka toleo hili huwa sio imara sana kwani ni maalum kwaajili ya majaribio.

Na hayo ndio mabadiliko ya app mpya ya Tanzania Tech, kupata habari zaidi kuhusu app yetu hakikisha unatembelea tovuti ya Tanzania Tech na pia unatufuata kwenye mitandao ya kijamii.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.