in

Video : Huu Hapa Ubora na Ugumu wa Samsung Galaxy Note 9

Fahamu kuhusu ugumu wa simu mpya ya Samsung Galaxy Note 9

Ugumu wa Samsung Galaxy Note 9

Kampuni ya Samsung hivi karibuni imezindua simu mpya ya Samsung Galaxy Note 9, sasa basi kama wewe ni mpenzi wa simu za Samsung, na Kama ulikua unataka kununua simu hiyo mpya ya Samsung Galaxy Note 9 ni vyema kusoma makala hii kwanza.

Kupitia makala hii utaweza kujua ubora na ugumu wa simu hii mpya na pia utaweza kujua je ni simu itakayo kufaa kulingana na maisha yako ya kila siku au lah.. Kujua zaidi nakushauri hakikisha una angalia video zote hapo chini…

Usiwe na haraka sana, kama kweli unataka kununua simu hii ni muhimu sana yani sana kuangalia video inayofuata hapo chini… Video hii inaonyesha ubora wa simu hiyo hasa kwa matumizi ya kawaida ya kila siku.

Ni matumaini yangu kuwa mpaka sasa umeshajua kama ununue au usinunue simu hii mpya. Kwa upande wangu mimi naona Samsung imejitahidi sana kwani ukiangalia video ya kwanza hapo juu utaona majaribio yalio kuwa yakifanyika ni majaribio ya kupiga na nyundo. Ni wazi kitendo hicho sio kitendo cha matumizi ya kila siku hivyo ni wazi kuwa Samsung Note 9 itaweza kuimili misukosuko ya maisha ya kila siku ya kitanzania.

Kampuni ya Airtel ya Kwanza Kuja na eSIM Tanzania

Kitu ambacho nimeona ni tatizo kwenye Galaxy Note 9 ni kupitia video ya pili, video ya pili imeonyesha kuwa vitufe vya Galaxy Note 9 vinaweza kutoka kwa urahisi hivyo ni wazi kuwa makini hasa pale unapo angusha simu hiyo kwani ni wazi kuwa inaweza isivunjike lakini vitufe vyake vya kuongeza sauti pamoja na kitufe cha kuwasha vikabanduka kabisa.

Kwa upande wangu ni hayo tu.. Hebu niambie kwa upande wako..? unaonaje ugumu wa simu hii mpya ya Samsung Galaxy Note 9. Tuambie kwenye sehemu ya maoni hapo chini.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.