in

Njia Mpya ya Kutengeneza Pesa Mtandaoni Kupitia Simu Yako

Utaweza kulipwa kupitia njia za kifedha za M-Pesa, Tigo Pesa na nyingine

pesa mtandaoni kupitia simu

Hapa Tanzania Tech tayari tumeshawahi kuongelea njia mbalimbali za kupata pesa mtandaoni ikiwa pamoja na njia za kuanza biashara mtandaoni. Lakini njia zote hizo ambazo tumewahi kuzionyesha kwa namna moja ama nyingine ni lazima itakuta inahusisha tovuti au application ya nje ya nchi hivyo mara nyingi unakuta kama unataka kulipwa ni lazima utalipwa kwa dollar.

Ukweli ni kwamba dollar ni nzuri sana, lakini sio kila mtu mwenye njia ya kuweza kupokea pesa hizo. Tunajua kuwa mara nyingi ili kuweza kupokea hela zako ambazo umetengeneza mtandaoni inakubidi kuwa na akaunti ya benki na tukubaliane na ukweli kuwa, sio watanzania wote wenye uwezo wa kuwa na akaunti za benki na hii ni kutokana na sababu mbalimbali.

Sasa kuliona hili, leo Tanzania Tech tunakuletea njia mpya na rahisi ya kuweza kutengeneza pesa mtandaoni kwa kutumia simu yako ya mkononi. Mbali ya njia hii kuwa rahisi, vilevile pia unaweza kutoa pesa zako kupitia huduma za kifedha za Tigo Pesa, M-Pesa na nyingine. Sasa kabla ujachoka moja kwa moja twende tuangalie njia hii rahisi.

Jinsi ya Kupata FREE Hosting Mwaka Mzima (Bure 100%)

Njia hii inahusisha watumiaji wa simu za Android,na vilevile njia hii inahusisha wewe kupakua application. Kama uko tayari unaweza kubofya link hapo chini itakupeleka kwenye soko la Play Store kisha pakua app hiyo kisha fuata maelezo hapo chini.

App hii ya premise ni app kutoka nje ya nchi ambayo inakupa uweza wa kujibu maswali mbalimbali ambayo utakuwa unalipwa kwa kujibu maswali hayo. App hii inakuja kwa lugha kiswahili pia na inakupa uwezo wa kutuma pesa zako utakazo zipata kupitia huduma za kifedha kupitia simu yako ya mkononi.

Ili kutumia App hii unatakiwa kuwasha GPS kwenye simu yako kwani ni muhimu ili kuweza kujua eneo ambalo unapatikana kwani hii itarahisha kukupatia maswali yanayo lingana na eneo ulilopo. Baada ya hapo unachotakiwa ni kuchagua lugha au app inaweza kugundua yenyewe na kukuletea kishwahili, kisha baada ya hapo sajili akaunti na utaletewa maswali ambayo ndio unatakiwa kujibu ili kupata pesa mtandaoni kupitia simu yako.

Jinsi ya Kutengeneza Dollar $3 au $5 Mtandaoni (Njia Rahisi)

Kila swali linakuja na gharama yake hivyo kama swali linahitaji mambo mengi zaidi basi ndivyo hivyo utakavyo lipwa zaidi. Vilevile maswali hayo yana muda maalum hivyo ni muhimu kuyajibu haraka kabla ya muda huo kuisha.

Baada ya kujibu maswali hayo inakubidi kusubiri kati ya siku moja au siku mbili na utawekewa pesa yako kupia app hiyo. Baada ya kuwekewa utaona pesa hiyo kwenye sehemu ya Payment na baada ya kufikisha kiwango kinachotakiwa utakuwa unaweza sasa kutoa kupitia njia mbalimbali za kifedha.

Na hiyo ndio njia mpya ambayo nimekuandalia leo ambayo unaweza kuitumia kutengeneza pesa mtandaoni kwa kutumia simu yako ya Android. Kumbuka njia hii haito kupa mamilioni bali kwa muda utaweza kutengeneza pesa kwaajili ya mambo mbalimbali kwenye maisha yako ya kila siku. Kama kuna mahali umekwama unaweza kutuandikia kupitiasehemu ya maoni hapo chini nasi tutakusaidia.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

41 Comments