in

Video : Muonekano wa Simu Mpya ya Infinix Note 5

Fahamu kwa undani sifa na muonekano halisi wa simu ya Infinix Note 5

Muonekano wa infinix-note-5

Hivi karibuni kampuni ya Infinix imezindua simu mpya ya Infinix Note 5, simu hii ni moja kati ya simu nzuri sana kutoka kampuni ya Infinx na ni moja kati ya simu yenye maboresho makubwa ukitofautisha na simu ya Infinix Note 4 ya mwaka jana 2017.

Kupitia Tanzania Tech leo nimepata nafasi ya kuweza kuiona kwa ukaribu simu hii na ukweli ni simu nzuri sana na kwa mwaka huu 2018, japokuwa simu hii inakuja na mfumo wa Android One ambao mfumo huu unakuja na programu maalum za Google pekee, lakini kampuni ya Infinix imefanikiwa kuweka programu zake ambazo kiukweli zinasumbua lakini kizuri ni kuwa unaweza kuziondoa programu hizo kwenye simu hiyo.

Simu hii pia inakuja na kamera nzuri yenye Megapixel 12 kwa nyuma na Megapixel 16 kwa mbele hii ikiwa inakupa nguvu zaidi kuweza kupiga picha zake za selfy vizuri kabisa. Mengineyo unaweza ukayafahamu kwa kuangalia video hapo chini.

Kampuni ya TECNO Yazindua Rasmi Spark 10 PRO

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

One Comment