in

Kampuni ya Oppo Yazindua Simu Mpya ya Oppo A5

Zifahamu Hizi hapa ndio sifa na bei ya simu mpya ya Oppo A5

Sifa na Bei ya Oppo A5

Baada ya kuzindua Oppo Find X, Kampuni ya Oppo imerudi tena na simu yake mpya ya daraja la kati, simu hii mpya ya Oppo A5 inakuja na muonekano mzuri sana na inakuja na sifa nzuri sana ukilinganisha na simu nyingine zenye majina makubwa.

Oppo A5 inakuja na kioo cha LCD chenye inch 6.2 na resolution ya 1520×720 pixel pamoja na aspect ratio ya 19.9. Simu hii pia inakuja na ukiongo wa juu maarufu kama Top Notch.

Kwa upande wa processor, simu hii mpya ya Oppo A5 inakuja na processor yenye chipset ya Snapdragon 450 pamoja na CPU ya octa-core ambayo inakuja na speed ya 1.8GHz. Simu hii pia inakuja na RAM ya GB 4 na GB 3, huku ikisaidiwa na ukubwa wa ndani wa GB 64 ambao unaweza kuongezwa kwa kutumia memory card hadi ya GB 256.

Kwa nyuma ya simu hii kuna kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 13 yenye f/2.2 na nyingine ikiwa na Megapixel 2 yenye f/2.4. Kwa mbele Oppo A5 inakuja na kamera ya kawaida yenye uwezo wa Megapixel 8 kwaajili ya kuchukua picha zako za kawaida za selfie. Sifa nyingine za Oppo A5 ni kama zifuatazo.

Sifa za Oppo A5

 • Ukubwa wa Kioo  – Inch 6.2 chenye teknolojia ya IPS LCD capacitive touchscreen, chenye uwezo wa kuonyesha rangi miloni 16 pamoja na resolution ya 720 x 1520 pixels, 19:9 ratio (~271 ppi density).
 • Mfumo wa Uendeshaji – Android One 8.1 (Oreo)
 • Uwezo wa Processor – Octa-core 1.8 GHz Cortex-A53, Qualcomm SDM450 Snapdragon 450 Chipset.
 • Uwezo wa GPU – Adreno 506
 • Ukubwa wa Ndani – GB 64 ikiwa na uwezo wa kuongezewa na memory card hadi ya GB 256.
 • Ukubwa wa RAM – GB 4 au GB 3
 • Uwezo wa Kamera ya Mbele –  Megapixel 6.
 • Uwezo wa Kamera ya Nyuma – Ziko kamera mbili moja ikiwa na Megapixel 13 yenye f/2.2, AF na nyingine ikiwa na Megapixel 2 yenye f/2.4, haina AF, depth sensor. Kamera zote mbili zinasaidiwa na flash ya LED Flash.
 • Uwezo wa Battery – Battery isiyotoka ya Li-Ion 4230 mAh battery.
 • Viunganishi – Wi-Fi 802.11 a/b/g/n, dual-band, WiFi Direct, hotspot, Bluetooth 4.2, A2DP, LE pamoja na GPS ya A-GPS, microUSB 2.0, USB On-The-Go.
 • Rangi – Inakuja kwa rangi mbili za Blue na Pink
 • Mengineyo – Inayo Radio FM, Inatumia Line Mbili za Dual SIM (Nano-SIM, dual stand-by), Inayo sehemu ya kuchomeka headphone maarufu kama Headphone jack.
 • Uwezo wa Mtandao – 2G, 3G na 4G
 • Ulinzi – Haina Ulinzi kwa Fingerprint. Inayo Teknolojia ya kutambua uso.
Kampuni ya Nokia Kubadilisha Logo Yake ya "NOKIA"

Bei ya Oppo A5

Simu hii mpya ya Oppo A5 kwa sasa bado haija anza kuuzwa rasmi ila unaweza kuipata kwa kutoa oda kwani mauzo ya simu hii yanatarajiwa kuanza tarehe 13 ya mwezi huu, huku simu hiyo ikitarajiwa kuuza kwa Yuan ya China CNY 1500 sawa na Shilingi za Tanzania Tsh 515,000. Kumbuka bei hiyo ni maalum kwa nchini China hivyo kwa hapa Tanzania bei inaweza kuongezeka.

Na hizo ndio sifa za Oppo A5, Je wewe umeonaje simu hii..? ni moja kati ya simu ambazo ungependa kuwa nayo mwaka huu 2018..? Tuambie kupitia sehemu ya moani hapo chini.

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

6 Comments