in

WhatsApp Kuja na Programu Mpya Kwaajili ya Kompyuta

Programu mpya ya WhatsApp kwenye kompyuta za Windows

WhatsApp Kwenye Kompyuta Windows

WhatsApp ni moja kati ya Application inayotumiwa sana na watu wengi, lakini pamoja na kutumiwa kwa wingi, bado kuna wakati mgumu kwa watumiaji wa kompyuta za Windows kuweza kutumia programu hiyo kwa urahisi. Hivi sasa ili kutumia WhatsApp kwenye kompyuta yako ni lazima kutumia kivinjari (Browser) kwenye kompyuta yako ndipo uweze kuunganisha programu ya WhatsApp kwenye simu yako na kompyuta yako.

Sasa hivi karibuni, inasemekana kuwa WhatsApp na kampuni ya Microsoft wanashirikiana ili kuleta programu mpya kabisa ya WhatsApp ambayo itakuwa ni kwa ajili ya watumiaji wa kompyuta za Windows. Hata hivyo kwa mujibu wa tovuti ya Thenextweb, tayari kumesha vuja picha inayosemekana kuwa ndio utakuwa muonekano wa programu hiyo mpya ya WhatsApp.

Hata hivyo pamoja na kuwepo kwa picha hii, bado ripoti hizi hazina uhakika na bado hatujajua tovuti yoyote iliyopata maelezo kutoka kwa wasemaji wa kampuni ya Microsoft au Facebook. Kupata ripoti kamili juu ya ujio wa programu hii endelea kutembelea Tanzania Tech tutakujulisha pindi tutakapo pata ripoti kamili.

Apps Nzuri Kwa Simu za Android Zilizopo Rooted

Written by Amani Joseph

Tanzania Tech tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate kwenye mitandao ya kijamii.

Toa Maoni Hapa

Kumbuka ni Muhimu Kuandika Jina Halisi na Barua Pepe, Vigezo na Masharti Kuzingatiwa.

2 Comments